Monday, January 16, 2017

#KUJIKUBALI NI HATUA KUBWA SANA NA YA KWANZA KATIKA MAISHA ILI MTU AWEZE KUFURAHIA UUMBAJI WA MUNGU.

#Hivi unamkubali kwa asilimia ngapi huyo unayemwona kwenye Kioo unapojiangalia?
#Kuna waliojikatia tamaa kabisa, hawataki hata kuona Rangi yao ya Ngozi, wanasahau ya kwamba HAKUNA ALIYEANDIKA BARUA KWA MUNGU ILI AZALIWE HIVYO ALIVYO. MUNGU ALIWAFANYIA SURPRISE WAZAZI WAKO

#JIKUBALI

Hamna haja ya Kujichubua ili uwe mweupe, hatuoi ngozi.
-Hamna haja ya kukuza makalio yako ili yatikisike unapotembea.
-Hamna haja ya kudharau nywele zako, kucha zako, kope za macho, na kuona za watu Fulani wa Ulaya na Amerika ndiyo zinafaa. JIKUBALI

#I MYSELF, I PREFER NATURAL WOMAN MORE THAN THE ARTIFICIAL ONE.

ACHA KUSUMBUKIA MAMBO AMBAYO WAOAJI HAWATAKI. WAZINZI NDIYO WANATAKA HAYO MADOIDO.

#STOP EDITING YOUR BODY
#STOP BEING CHEAP TO MEN
#START BEING EXPENSIVE FROM THIS TIME ON.

MUNGU alimwumba Mwanadamu akiwa kamili. ULIUMBWA KWA SURA NA MFANO WA MUNGU.
#NI HESHIMA KUBWA SANA AMBAYO MUNGU ALIKUPATIA, KUPEWA MWONEKANO WAKE-MFANO WAKE NA SURA YAKE.

Kuna Watu wengi sana sahivi duniani ambao wamejitolea Kubadili Sura zao na Mfano wao kuwa kama Watu Fulani hivi ambao ni Maarufu-By the name of Role Models.

*Usiwe kama Michael Jackson ambaye aliona Rangi ya ngozi yake na mwonekano wake haumtoshelezi.
*You're an Image of God. Be Proud of that

#Jikubali
-Acha Kuhangaika na Vipodozi. Wewe ni Mzuri, Uzuri uliwekwa ndani yako tangu siku Ulipoumbwa na Mungu katika Fikra zake.

HUWEZI KUWA MJANJA KULIKO MUNGU. LABDA UJIFANYE TAIRA

Haya Mambo ya watu Kurekebisha uumbaji wa Mungu katika Miili yao ulikuwepo hata zamani wakati wa mfalme Sulemani. Mfalme Sulemani anasema,

#Tazama hili tu nimeliona; MUNGU AMEMFANYA MWANADAMU MNYOFU, LAKINI WAMEBUNI MAVUMBUZI MENGI (Mhubiri 7:29)

Walioleta Nywele bandia, kucha na kope za bandia, Vipodozi, dawa za kukuza/kupunguza matiti au Makalio, na hayo unayoyajua wewe NI MAVUMBUZI MENGI YALIYOBUNIWA NA WANADAMU.


#GOD MADE A PERFECT MAN JUST AS HE IS. MEN SAW THEMSELVES NOT PERFECT BECAUSE OF SIN WITHIN THEM-Lackson Tungaraza.

DHAMBI HUMFANYA MTU AJIONE AMEPUNGUKIWA MAMBO FULANI HIVI ILI ATEKE MVUTO KWA WENGINE

KABLA YA ADAMU NA HAWA KUTENDA DHAMBI YA UASI WALIKUWA UCHI SIKU ZOTE NA WALIJIONA WA KAWAIDA TU.
#DHAMBI ilipoingia ndani Yao, wakaona ya kwamba kuna mambo Fulani hivi ambayo yamepungua kwenye Miili yao
-Wakajiona wako Uchi, wakajifunika kwa matawi.

Dhambi umekufanya Usijikubali.SHETANI KAKUAMBIA NYWELE ZAKO, NGOZI YÀKO, KUCHA ZÀKO, UMBO LAKO SIYO SAHIHI. UMEDANGANYIKA NA. KUREKEBISHA UZURI ULIOKUWA NDANI YAKO.

#JIKUBALI
*TUBU DHAMBI ILIYOJIFICHA NDANI YAKO. DHAMBI NI MBAYA SANA

KUTOKUJIKUBALI NI UTUMWA MBAYA SÀNA MAANA NI WÀ NDANI KWA NDANI, SIYO WÀ MINYORORO NA PINGU

#JIKUBALI. YOU ARE SPECIAL AND UNIQUE, FULL OF GOD's BEAUTY

ZAIDI PATA KITABU CHA #FICHUKA Ujifunze zaidi.

Kingdom Transformer,
Lackson Tungaraza
0764793105-whatsapp or Call

Open.. http://lacksontungaraza.blogspot.com

www.facebook.com/ltungaraza

FIX ME JESUS

Related Posts:

  • NJIA MPYA YA KUTENGENEZA KIPATO CHA ZIADAHaijalishi una Kazi ama hauna Kazi, kikubwa ni UTAYARI wako pamoja na Kiasi kidogo cha #PESA kuanzia Tsh.4000/= Sasa Unaweza Kutengeneza Kipato cha Ziada (PESA) kupitia Kitabu changu "SITARUDI NYUMA TENA" - Sitaki KUFANIKI… Read More
  • HATUA ZA MAFANIKIO "MAFANIKIO hayaji kwa Ukubwa au Udogo wa kile Ulichonacho, bali kwa namna Unavyotumia kile Ulichonacho" ~Lamax Kila siku nikikumbuka Hatua nilizopitia Kufika hapa nilipo Leo Kimaisha, ninapata hamasa ya Kumshukuru Mungu k… Read More
  • FIND_SOMETHING_TO_DIE_FOR_THAN_TO_LIVE_FOR FANYA JAMBO la Kumfanya MUNGU azidi Kuona  Umuhimu wa Kukuacha Uendelee kuwa HAI hapa duniani. JAMBO la Kumfanya MUNGU aone KUNA PENGO wakati  wa Kuugua Kwako (Kupatwa na Magonjwa) ili AKUPONYE HARAKA URUDI… Read More
  • BADO UNAENDELEA KUVUNJA LAANA ZA UMASKINI? Tangu Uanze kuvunja Laana za UMASKINI, huu ni Mwaka wa ngapi, na Je Umeshaanza kuwa TAJIRI? Kabla ya Kuanza au Kuendelea tena na Uvunjaji Wako wa Laana za UMASKINI, Tathimini Kwanza ni kwa Jinsi Umejitoa Kulipa Gharama … Read More
  • UNAMALIZAJE HUU MWAKA WA 2017?? Kati ya maeneo ambayo huwa yanawatia watu Joto Kubwa ni eneo la Umalizaji. Umalizaji huu huenda mbali zaidi katika mchezo wa Mpira, katika Utumishi, kwenye Chumba cha Mitihani, kwenye Ndoa, Uchaguzi Mkuu n.k... Eneo hili hu… Read More

1 comment:

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI