Thursday, December 31, 2015

UHUSIANO KATI YA PESA NA MALENGO


Natoa shukurani zangu za dhati kwako msomaji wa makala zangu za uelimishaji kupitia blog yangu lacksontungaraza.blogspot.com , kupitia page yangu ya Facebook inayoitwa Network Marketing Business na kupitia mitandao mingine ya kijamii ndani ya mwaka huu mzima wa 2015. Kwa hakika wewe ni mtu wa muhimu sana kwangu na ndiyo maana nazidi kupata hasa ya kuandika zaidi na zaidi kila mara. Kutokana na kuwepo kwa matatizo ya watu kutokujua uhusiano uliyopo kati ya pesa na malengo, hivyo nimeamua kuweka mada hii mezani ili kuleta ufafanuzi kwa kina. Ni kweli unatamani kupata fedha kwa kila njia, je unafahamu uhusiano uliopo kati ya pesa unayoitafuta na Malengo yako kibiashara au kimaisha kwa ujumla?

Malengo ni ile mikakati ambayo mtu binafsi amejiwekea ili aweze kuitimiza ndani ya muda fulani bila kujali hali aliyonayo kwa wakati huo, inaweza kuwa hali ya kiuchumi au vinginevyo.
Nakumbuka nilipokuwa kidato cha pili, kuna watu walikuwa wakiniambia kuwa kidato cha tatu ni kigumu sana kwa sababu ya ugumu wa masomo na wingi wa mitihani. Lakini niliweza kuamini malengo yangu ya kufaulu kwa kishindo bila kujali ni nani kasema nini, na mwisho wa siku nikawa mwanafunzi wa ufahulu wa kwanza kidato cha nne kwa mwaka huo katika shule yetu.
Huo ni mfano tu wa malengo lakini hayakuwa ya kifedha, bali ya kielimu ya darasani. Tunapokuja katika suala la kiuchumi, malengo pia ni muhimu sana kuliko hata mikopo unayoangaikia usiku na mchana. Malengo ndiyo dira.

Kuna siku moja ya Jumapili baada ya kutoka ibadani mjini Dodoma, nilianza kuwashirikisha vijana wenzangu elimu ya fedha. Niliweza kumuuliza mmoja swali lifuatalo, “Je leo nikikupatia laki tano, ni biashara gani ambayo utaifanya kujikwamua kiuchumi? ”. Lakini nilishangazwa na jibu lake “Endapo nikipata hiyo fedha kwa sasa, nitaangalia ni biashara gani inayolipa kwa sasa mjini.” Kilicho nishangaza  ni kwamba alikuwa na shauku sana ya kupata fedha ya kufanyia biashara kwa sababu amechoswa na maisha ya kuwa tegemezi lakini hakuwa na Malengo.

Mara nyingi watu wanaangaika kuonga bank na katka taasisi mbali mbali za mikopo ili wapate fedha ya kujikimu kimaisha kwa kufanya biashara lakini hawana malengo stahiki ya kuthaminisha na kuikuza hiyo pesa.
Ebu leo chukua kipande kidogo cha karatasi na uandike Malengo yako hata mawili ambayo ungependa kabla ya mwaka 2015 hujaisha uwe umeyatimiza au ukaanza nayo tarehe 1 Januari 2016 bila kupoteza muda, kisha tafuta hiyo fedha ya kuwezesha malengo hayo.


Tangu nimeanza biashara ya kisasa  “network marketing”  nimegundua mambo mengi ikiwemo hili la upangaji wa malengo kibiashara. Pia nawe unaweza endapo utaamua na kuamini kutoka katika vilindi vya moyo wako. Usisahau kuchangia mawazo yako hapa ili tujenge jamii iliyo imara kiuchumi na kimtazamo,  ungana na Email list yangu kwa kutuma email yako kwenye Email yangu lacksontungaraza@gmail.com ili uzidi kupata masomo mbali mbali moja kwa moja. Kwa mawasiliano zaidi, SMS/call/whatsapp 0764793105 (Lackson Tungaraza). Tukutane katika mada zitakazofuata ambazo ni moto moto zaidi.

Related Posts:

  • UJASIRIAMALI NI NINI? Kuna tafsiri mbali mbali katika vichwa vya watu na katika mitandao ya kijamii juu ya dhana ya UJASIRIAMALI. Wengi wamepata tafsiri zilizowapa presha na kuamua kuacha kuwa WAJASIRIAMALI, na baadhi hawatambua ni kwa namna gan… Read More
  • MAMBO MATATU MUHIMU YA KUFANYA KIJANA KABLA YA KUANZA KUTAFUTA PESA YA KUFANYA BIASHARA Kijana mwenzangu kabla hujaanza kusumbuka kutafuta pesa kila mahala kwaajili ya biashara.  Kwanza Fanya maamuzi ni biashara gani unayohitaji kufanya, hiyo ni hatua ya kwanza kabisa. Kwanini ufanye uwamuzi kwanza? Ili k… Read More
  • SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA  “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA”  Tunashindwa kuongeza vipato vyetu kwa sababu biashara zetu hazina mvuto. Tunapoendelea kufungua vyanzo vingine vya vipato kwa kut… Read More
  • MTAJI KWA KIJANA NI UPI...! Proudly Sponsored by N.Y.I MOVEMENT *Join and Be part of the Change*. Kuna mambo mbali mbali ambayo wewe kama Kijana mwenzangu unaweza fanya pasipokuwa na pesa kubwa Bali hiyo hiyo uliyonayo hapo .... Akili, maarifa… Read More
  • UKWELI JUU YA SEMINA ZA MTANDAONI Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu tele, una ndugu, una marafiki wazuri, umekul… Read More

1 comment:

  1. Kwa kujua mbinu hii kabla ya kupata fedha, utashangaa matokeo yake

    ReplyDelete

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI