CHAGUA LEO
UNAPENDA KUWA KAMA NANI MAISHANI
Kama wewe ni
Mzazi, ni rahisi sana mtoto wako kutamani kuwa kama wewe kitabia au
kimafanikio. Utamsikia mtoto akisema maneno kama, “nataka nije kuwa daktari
kama baba au mama, nataka niwe nashika majambazi kama baba ” n.k. Vivyo hivyo
kupitia waalimu wanaomfundisha shuleni, anaweza kupenda jinsi mwalimu wake
alivyo na jinsi anavyofundisha na kutamani siku moja kuwa hivyo.
Nakumbuka nilianza
kupata hamasa ya kutafuta njia za kupata mafanikio kwa kutumia ujuzi na kipawa
ambacho Mungu ameweka ndani yangu kupitia mafunzo ya Bwana Robert Kiyosaki, ambaye ni Mwandishi mkubwa wa vitabu
mbalimbali vya Uwekezaji, Kujitambua, Elimu ya biashara n.k. Moja ya kitabu
kilichompa umaarufu hadi sasa ni kitabu cha “RICH DAD POOR DAD”. Lakini pia
kuna kitabu cha Wajasiriamali waliofanikiwa kiitwacho “MIDAS TOUCH” kumfundisha
Mjasiriamali mambo matano ambayo anapaswa kuwa nayo ili kufanikiwa, na vitabu
vingine vingi kama “Unfair Advantage” na “Second Chance”. Kwa jinsi ambavyo ameelezea
safari yake ya mafanikio kutoka katika mazingira magumu hadi kuwa Milionea
ilinipa nguvu sana na hamasa na tangu kipindi hicho niliweza kujitambua na
kuamini ipo siku na mimi nitapiga hatua fulani kimaisha. Hata wewe pia unaweza,
tambua hazina iliyoko ndani yako kupitia somo hili na kwenye vitabu mbalimbali.
Vivyo nikaanza kutamani kuwa kama huyu jamaa kimafanikio, japokuwa safari bado
ni ndefu lakini naamini nitafika tu kwa neema ya Mwenyezi Mungu atupae yote.
Lackson Tungaraza |
Hicho ndicho
nilichotaka kukizungumzia leo. Ukweli ni kwamba watu wengi sana ambao unawaona
wana mafanikio makubwa sana, wana watu wao ambao waliwaweka mbele. Kwa mfano,
wewe unafanya biashara, je ni mfanya biashara gani mkubwa ambaye ungependa uwe
kama yeye? Je, umedhamiria kweli kufikia mafanikio aliyo nayo huyo “Role Model”
wako?
Kama wewe ni
Mwanafunzi , ungetamani siku
moja uwe kama msomi gani mashuhuri nchini? Kama unacheza mpira, ni mchezaji
gani maarufu ambaye siku moja utafurahi ukiwa katika kiwango chake na kufikia
mafanikio yake? Hilo ni jambo la msingi sana la kulifanyia kazi ili uweze
kuongeza jitihada katika fani unayotarajia ikufikishe kwenye ulimwengu wa
mafanikio.
Ukiwa
mafanyabiashara na ukatamani uwe na mafanikio makubwa kama aliyonayo Saidi
Bakhresa, lazima utakuwa na nidhamu katika fedha zako na utatumia mbinu sahihi
za kibiashara ambazo mfanyabiashara huyo ametumia.
Uzuri ni kwamba,
watu wengi wenye mafanikio, historia zao zinapatikana. Baadhi maisha yao yapo
kwenye vitabu, wengine kwenye vitabu, wengine kwenye mitandao, hivyo ni rahisi
sana kujifunza nini walikifanya mpaka kufikia walipo, changamoto walizopitia na
jinsi walivyokabiliana nazo. Mfano hai wa hapa nchini ni Bwn. Erick Shigongo
ambaye alikuwa amemtanguliza mbele mfanyabiashara mkubwa sana, Reginald Mengi
kama “role model” wake. Je, wewe ungependa kuwa kama nani? Je ,kuna mtu ambaye
unafuata nyayo zake? Kama unataka kuwa kama Shigongo, je unajua alikopitia
mpaka alipo sasa? Wewe pia amini siku moja unaweza kuwa kama Fulani ambaye ana
mafanikio makubwa kama tu utakuwa na dhamira ya kweli. Hebu changia mawazo
yako hapa kwa jinsi ulivyojifunza
kupitia hii mada.
ukiwa na role model mzuri, hutojutia hiyo safari yako..
ReplyDeletenini maoni yako juu ya hili?