UHUSIANO KATI YA PESA
NA MALENGO
Natoa shukurani zangu
za dhati kwako msomaji wa makala zangu za uelimishaji kupitia blog yangu
lacksontungaraza.blogspot.com , kupitia page yangu ya Facebook inayoitwa
Network Marketing Business na kupitia mitandao mingine ya kijamii ndani ya
mwaka huu mzima wa 2015. Kwa hakika wewe ni mtu wa muhimu sana kwangu na ndiyo
maana nazidi kupata hasa ya kuandika zaidi na zaidi kila mara. Kutokana na
kuwepo kwa matatizo ya watu kutokujua uhusiano uliyopo kati ya pesa na malengo,
hivyo nimeamua kuweka mada hii mezani ili kuleta ufafanuzi kwa kina. Ni kweli
unatamani kupata fedha kwa kila njia, je unafahamu uhusiano uliopo kati ya pesa
unayoitafuta na Malengo yako kibiashara au kimaisha kwa ujumla?
Malengo ni ile mikakati
ambayo mtu binafsi amejiwekea ili aweze kuitimiza ndani ya muda fulani bila
kujali hali aliyonayo kwa wakati huo, inaweza kuwa hali ya kiuchumi au vinginevyo.
Nakumbuka nilipokuwa
kidato cha pili, kuna watu walikuwa wakiniambia kuwa kidato cha tatu ni kigumu
sana kwa sababu ya ugumu wa masomo na wingi wa mitihani. Lakini niliweza
kuamini malengo yangu ya kufaulu kwa kishindo bila kujali ni nani kasema nini,
na mwisho wa siku nikawa mwanafunzi wa ufahulu wa kwanza kidato cha nne kwa
mwaka huo katika shule yetu.
Huo ni mfano tu wa
malengo lakini hayakuwa ya kifedha, bali ya kielimu ya darasani. Tunapokuja
katika suala la kiuchumi, malengo pia ni muhimu sana kuliko hata mikopo
unayoangaikia usiku na mchana. Malengo ndiyo dira.
Kuna siku moja ya
Jumapili baada ya kutoka ibadani mjini Dodoma, nilianza kuwashirikisha vijana
wenzangu elimu ya fedha. Niliweza kumuuliza mmoja swali lifuatalo, “Je leo nikikupatia laki tano, ni biashara
gani ambayo utaifanya kujikwamua kiuchumi? ”. Lakini nilishangazwa na jibu
lake “Endapo nikipata hiyo fedha kwa
sasa, nitaangalia ni biashara gani inayolipa kwa sasa mjini.” Kilicho nishangaza ni kwamba alikuwa na shauku sana ya kupata fedha
ya kufanyia biashara kwa sababu amechoswa na maisha ya kuwa tegemezi lakini hakuwa na Malengo.
Mara nyingi watu
wanaangaika kuonga bank na katka taasisi mbali mbali za mikopo ili wapate fedha
ya kujikimu kimaisha kwa kufanya biashara lakini hawana malengo stahiki ya
kuthaminisha na kuikuza hiyo pesa.
Ebu
leo chukua kipande kidogo cha karatasi na uandike Malengo yako hata mawili
ambayo ungependa kabla ya mwaka 2015 hujaisha uwe umeyatimiza au ukaanza nayo
tarehe 1 Januari 2016 bila kupoteza muda, kisha tafuta hiyo fedha ya kuwezesha
malengo hayo.
Tangu
nimeanza biashara ya kisasa “network
marketing” nimegundua mambo mengi
ikiwemo hili la upangaji wa malengo kibiashara. Pia nawe unaweza endapo utaamua
na kuamini kutoka katika vilindi vya moyo wako. Usisahau kuchangia mawazo yako
hapa ili tujenge jamii iliyo imara kiuchumi na kimtazamo, ungana na Email list yangu kwa kutuma email
yako kwenye Email yangu lacksontungaraza@gmail.com
ili uzidi kupata masomo mbali mbali moja kwa moja. Kwa mawasiliano zaidi, SMS/call/whatsapp 0764793105 (Lackson Tungaraza). Tukutane katika mada
zitakazofuata ambazo ni moto moto zaidi.
Kwa kujua mbinu hii kabla ya kupata fedha, utashangaa matokeo yake
ReplyDelete