Sunday, December 27, 2015

  CHAGUA LEO UNAPENDA KUWA KAMA   NANI MAISHANI






Kama wewe ni Mzazi, ni rahisi sana mtoto wako kutamani kuwa kama wewe kitabia au kimafanikio. Utamsikia mtoto akisema maneno kama, “nataka nije kuwa daktari kama baba au mama, nataka niwe nashika majambazi kama baba ” n.k. Vivyo hivyo kupitia waalimu wanaomfundisha shuleni, anaweza kupenda jinsi mwalimu wake alivyo na jinsi anavyofundisha na kutamani siku moja kuwa hivyo.

Nakumbuka nilianza kupata hamasa ya kutafuta njia za kupata mafanikio kwa kutumia ujuzi na kipawa ambacho Mungu ameweka ndani yangu kupitia mafunzo ya Bwana Robert Kiyosaki, ambaye ni Mwandishi mkubwa wa vitabu mbalimbali vya Uwekezaji, Kujitambua, Elimu ya biashara n.k. Moja ya kitabu kilichompa umaarufu hadi sasa ni kitabu cha “RICH DAD POOR DAD”. Lakini pia kuna kitabu cha Wajasiriamali waliofanikiwa kiitwacho “MIDAS TOUCH” kumfundisha Mjasiriamali mambo matano ambayo anapaswa kuwa nayo ili kufanikiwa, na vitabu vingine vingi kama “Unfair Advantage” na “Second Chance”. Kwa jinsi ambavyo ameelezea safari yake ya mafanikio kutoka katika mazingira magumu hadi kuwa Milionea ilinipa nguvu sana na hamasa na tangu kipindi hicho niliweza kujitambua na kuamini ipo siku na mimi nitapiga hatua fulani kimaisha. Hata wewe pia unaweza, tambua hazina iliyoko ndani yako kupitia somo hili na kwenye vitabu mbalimbali. Vivyo nikaanza kutamani kuwa kama huyu jamaa kimafanikio, japokuwa safari bado ni ndefu lakini naamini nitafika tu kwa neema ya Mwenyezi Mungu atupae yote.
Lackson Tungaraza


Hicho ndicho nilichotaka kukizungumzia leo. Ukweli ni kwamba watu wengi sana ambao unawaona wana mafanikio makubwa sana, wana watu wao ambao waliwaweka mbele. Kwa mfano, wewe unafanya biashara, je ni mfanya biashara gani mkubwa ambaye ungependa uwe kama yeye? Je, umedhamiria kweli kufikia mafanikio aliyo nayo huyo “Role Model” wako?

Kama wewe ni Mwanafunzi , ungetamani siku moja uwe kama msomi gani mashuhuri nchini? Kama unacheza mpira, ni mchezaji gani maarufu ambaye siku moja utafurahi ukiwa katika kiwango chake na kufikia mafanikio yake? Hilo ni jambo la msingi sana la kulifanyia kazi ili uweze kuongeza jitihada katika fani unayotarajia ikufikishe kwenye ulimwengu wa mafanikio.
Ukiwa mafanyabiashara na ukatamani uwe na mafanikio makubwa kama aliyonayo Saidi Bakhresa, lazima utakuwa na nidhamu katika fedha zako na utatumia mbinu sahihi za kibiashara ambazo mfanyabiashara huyo ametumia.


Uzuri ni kwamba, watu wengi wenye mafanikio, historia zao zinapatikana. Baadhi maisha yao yapo kwenye vitabu, wengine kwenye vitabu, wengine kwenye mitandao, hivyo ni rahisi sana kujifunza nini walikifanya mpaka kufikia walipo, changamoto walizopitia na jinsi walivyokabiliana nazo. Mfano hai wa hapa nchini ni Bwn. Erick Shigongo ambaye alikuwa amemtanguliza mbele mfanyabiashara mkubwa sana, Reginald Mengi kama “role model” wake. Je, wewe ungependa kuwa kama nani? Je ,kuna mtu ambaye unafuata nyayo zake? Kama unataka kuwa kama Shigongo, je unajua alikopitia mpaka alipo sasa? Wewe pia amini siku moja unaweza kuwa kama Fulani ambaye ana mafanikio makubwa kama tu utakuwa na dhamira ya kweli. Hebu changia mawazo yako  hapa kwa jinsi ulivyojifunza kupitia hii mada.

Related Posts:

  • UMUHIMU WA RATIBA KATIKA MAISHA YAKO Maisha ya Mwanadamu yana mwanzo na mwisho, ikiwa na maana ya kwamba kuna kuzaliwa na kufariki. Lakini katikati ya kuzaliwa na kufariki kuna mambo ambayo Mwanadamu anatakiwa afanye ili aweze kustahimili hali ya kimwili na… Read More
  • PATA MAARIFA KWA KUWA MKIMYA ~ Wanadamu hata siku moja haitawahi kutokea tukawa sawa kimtazamo, kimienendo..never. Unaweza ukajiulza mbona Mimi ninajiheshima, mpole, mvumilivu lakini huyu ndugu yangu ni mkorofi sana, mlevi, mbeya, mzinzi n.k. Hyo … Read More
  • UNAKIMBIA KWA STAILI GANI? Moja ya tafsiri za Maisha nilizowahi kuzisoma na kuzisikia ni kwamba Maisha ni Mbio. Cha kujiuliza, “Unakimbizana na nani?” Nimegundua ya kwamba Maisha ni Mbio ambayo Mshindani ni wewe mwenyewe… unajipulizia mwenyewe kipen… Read More
  • KUWA STARRING WA MAISHA YAKO. ~Nilipokuwa mtoto nilipendelea sana kutazama muvi za ngumi ( action movies), katika kuangalia kwangu nilishangaa kuona ya kwamba muhusika mkuu wa Muvi ambaye ndiye anaitwa STARRING alikuwa hafi hata kama amekutana na maj… Read More
  • LIFE IS A PROCESS [Maisha Ni Mlolongo Wa Mambo] Ni nini maana ya neno ‘Maisha?’ Kila mtu anaweza kutoa maana ya neno Maisha kwa yale aliyoyapitia, anayoyapitia au anayotarajia kukutana nayo mbeleni. Maisha yanamaana nyingi sana na kulingana na mtazamo wa kila mtu, ja… Read More

1 comment:

  1. ukiwa na role model mzuri, hutojutia hiyo safari yako..
    nini maoni yako juu ya hili?

    ReplyDelete

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI