Monday, December 14, 2015


Wahenga walisema,"UMOJA NI NGUVU" baada ya utafiti walioufanya katika nyanja mbalmbal ikiwemo kwa wadudu kama mchwa ambao licha ya udogo wao kimaumbile wanafanya maajabu kama ya kutengeneza vichuguu vikubwa na hata kula mbao na vitu mbalmbal vya thamani ambavyo ni vya aina hiyo.Hiyo yote kwa sababu ya "umoja" waliojijengea katika kazi.
Mara kwa mara tumekuwa tukikutana na wadudu njiani wakiwa kwenye misafara yao huku wamebeba nyasi, vijiti, maua n.k. kwa ajili ya ujenzi, chakula na matumizi mengine, kwa pamoja.

Katika nyanja ya biashara, pia mifano hiyo inahitajika ili kuweza kufanikisha kwa urahisi. chukulia mfano wa kawaida,ukiwa unahitaji kufyatua tofali 200 na ukawaalika rafiki zako 20 kukusaidia, kwa hakika hiyo shughuli utaimaliza kwa muda mfupi huku kila mtu akitumia nguvu kidogo. Lakini ikiwa mtu huyo huyo ataamua kufyatua tofali 200 mwenyewe, atatumia nguvu nyingi na muda mrefu kukamilisha hilo zoezi.

Biashara yoyote ile bila kujali ukubwa wake, ili ifanikiwe na kudumu kwa muda mrefu ni muhimu sana kuwa na UMOJA aidha wa mtu na mtu au taasisi na taasisi n.k. Hii ni kwa sababu kila mtu ana'nguvu' na 'udhaifu' wake, hivyo tunapokuja pamoja ule udhaifu unakuwa hauna nguvu wala kupata nafasi.Miongoni mwetu kuna watu ambao ni wazuri katika kupata mawazo mapya ya biashara lakini ni wadhaifu katika utekelezaji na wengine ni wazuri katika katika utendaji lakini hawana uwezo wa kupata mawazo mapya ya uendeshaji wa biashara n.k. Hivyo wakifanya shughuli pamoja wanaweza fika mbali sana ikiwa tu watafanya mambo yafuatayo;
1. Kutokuwa na majivuno
2. Kuwa na nidhamu na upendo

Chukulia mfano wa wafanya biashara wakubwa hapa nchini kama Bakhresa, Reginald Mengi na wengine wengi wameweza kupiga hatua kubwa kibiashara na kuliteka soko kwa muda mrefu kwa sababu ya UMOJA waliyoutengeneza na wafanya biashara wenzao na pia kufanya kazi na watu mbalmbal katika biashara zao wenye ujuzi mbalmbal kibiashara.

Watu wengi biashara zao hazikui au zinawahi kufa kwa sababu ya "Ubinafsi", wakidhani kila jambo wanaweza kulifanya na hata kama wakiliweza jambo hilo, unakuta muda mwingi umepotea hewani. Hivyo chukua notebook yako ukae sehemu tulivu utafakari haya;
1. Je, nina ushirikiano na wafanya biashara wenzangu wenye mitazamo chanya?
2. Je, nina penda kujifunza kwa waliotangulia kibiashara na kurekebisha makosa yao?
3. Je, biashara yangu inautofauti na biashara zingine ili kuleta mvuto kwa wateja?
Ukishapata majibu sahihi, chukua hatua. NGOJA NGOJA HUUMIZA MATUMBO.

Moja ya biashara ambazo kwa umoja na ushirikiano umewezesha wengi kufika mbali kiuchumi na kimtazamo ni biashara ya kisasa (Network Marketing). Lackson Tungaraza ni mmoja wa watu hao ambao wamepiga hatua kwa sababu ya kufanya biashara na watu wengine kwa umoja wakiwa na mitazamo chanya kwa pamoja.Unaweza wasiliana nae kwa sms/whatsapp kwa nambari 0764793105.

Hivyo kuanzia leo anza kutafuta rafiki wa kufanya nae biashara, lakini hakikisha pia nae ana mtazamo chanya na imani ya kuyafikia malengo yetu kwani wahuni ni wengi.

"USISAHAU, UMOJA NI NGUVU"
Au wewe unasemaje juu ya hili?..changia hapa na wengne wajifunze pia


UMOJA UNAFIKISHA WATU MBALI














Related Posts:

  • MTAJI KWA KIJANA NI UPI...! Proudly Sponsored by N.Y.I MOVEMENT *Join and Be part of the Change*. Kuna mambo mbali mbali ambayo wewe kama Kijana mwenzangu unaweza fanya pasipokuwa na pesa kubwa Bali hiyo hiyo uliyonayo hapo .... Akili, maarifa… Read More
  • WHY ONLINE SEMINARS? UKWELI JUU YA SEMINA ZA MTANDAONI Natumaini wewe ni mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Ni jambo jema sana la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia siku nyingine tena ukiwa na nguvu tel… Read More
  • SIRI AMBAZO MFANYA BIASHARA HUJAZIJUA  “JINSI YA KUFANYA BIASHARA YAKO KUWA YA TOFAUTI NA YENYE MVUTO MKUBWA”  Tunashindwa kuongeza vipato vyetu kwa sababu biashara zetu hazina mvuto. Tunapoendelea kufungua vyanzo vingine vya vipato kwa kut… Read More
  • MAMBO MATATU MUHIMU YA KUFANYA KIJANA KABLA YA KUANZA KUTAFUTA PESA YA KUFANYA BIASHARA Kijana mwenzangu kabla hujaanza kusumbuka kutafuta pesa kila mahala kwaajili ya biashara.  Kwanza Fanya maamuzi ni biashara gani unayohitaji kufanya, hiyo ni hatua ya kwanza kabisa. Kwanini ufanye uwamuzi kwanza? Ili k… Read More
  • FACEBOOK VS BLOG KIPI NI BORA KWA BIASHARA YAKO? Kumekuwa na sitofahamu juu ya namna ya kutumia mitandao hii katika kukuza biashara. Ndiyo maana nimekuuliza; Kati ya Facebook na Blog, ni kipi bora kwa Biashara yako? Jibu lako litaash… Read More

1 comment:

  1. Biashara za watu wengi zinachangamoto kubwa kutokana na ubinafsi na kukata tamaa mapema. Je wewe kwa mtazamo wako unawashauri nini wafanya biashara wengine?

    ReplyDelete

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI