Saturday, March 16, 2019

Watu Wengi huwa Wananunua Vifurushi vya Intaneti Ili Waelimike Mtandaoni, Lakini huwa hawafikii hayo Malengo Yao.

- Unakuta Mtu anaingia YouTube ili apate Elimu ya kumsaidia Kukua Kiroho au Kiuchumi, lakini anaishia kuangalia Comedy  (Vichekesho), Mieleka ya WWE, Video za Ngono  (Pornography), Udaku, Series, Taarifa ya Habari, N.k.



- KIFURUSHI KINAPOISHA, au kinapokaribia kuisha, ndipo Wanakumbuka walichokuwa wanataka Kujifunza. Na tabia hiyo hujirudia tena na tena baada ya Kununua Vifurushi vingine vya Intaneti. Nami Lackson Tungaraza nilikuwa Vivyo hivyo hapo Awali.


UNAJUA SHIDA NI NINI??

- SHIDA ni kwamba hawajui kwa Kina wanachotaka Kujifunza, kwa nini wanataka Kujifunza hicho wanachotaka Kujifunza  (Nia na Sababu ya kujifunza), na kutokuwa na Nidhamu binafsi (Self-Discipline) ya Kujiongoza.

Inawezekana kabisa nawe unayesoma huu ujumbe ni Muhanga  (Victim) wa hilo, Usihofu Ikiwa utaamua Kubadilika kuanzia Sasa. Sasa FANYA YAFUATAYO KABLA YA KUINGIA FACEBOOK, INSTAGRAM, YOUTUBE, N.K;

(I) Fahamu Unataka Kujifunza nini na kwa Nani (Mtu anayefundisha Unachokitaka, au Kama ni Page au Channel ya YouTube).

(II) Fahamu ni KWA NINI Unataka Kujifunza  (Nia na Sababu Yako ya Kujifunza).

(III) ANDIKA Mahali Yale Yote Unayotaka Kujifunza YouTube. Mfano!
- Jinsi ya Kutengeneza Sabini ya Unga.
- Faida za Nyama tamu ya Sungura. N.k.

(IV) Ingia Mtandaoni na kuanza kutekeleza hatua hiyo ya (III) hapo Juu. Ikiwa na maana ya kwamba UWE NA NIDHAMU BINAFSI YA KUJISIMAMIA, KUJIZUIA USIANGALIE au USIFANYE AMBAYO HUKUPANGA, na Kuweza KUJIONGOZA  (Leading Yourself).
Kumbuka kutumia "SEARCH BUTTON" (Kitufe cha Kutafutia unachokitaka) Kupata Yale uliyopanga Kujifunza YouTube.

(V) Ondoka Mtandaoni UKAFANYIE KAZI ULICHOJIFUNZA au ULICHOPAKUA MTANDAONI  (What you Downloaded from the Internet).


KWA KUFANYA HIVYO;

(I) Utakuwa unaokoa muda wako mwingi (Time saving).

(II)  Utakuwa unatumia vyema Vifurushi vya Intaneti kama ulivyokusudia. Na Pia

(III) Utakuwa Mbali na mambo yasiyokuhusu ambayo yangekupotezea Muda Wako na Kuharibu Tabia Yako njema - kwa Sababu Mazungumzo mabaya na Marafiki Wabaya huaribu tabia Njema.


Naamini Utakuwa umejifunza Jambo la Kukusaidia unapokuwa Mtandaoni. Usisahau kutendea kazi na Kushea hili Somo Zuri sana kwa Rafiki zako waliyopo Facebook, Messenger, Instagram, WhatsApp, Twitter, n.k. Uwe na Siku njema sana. Ni Mimi Rafiki Yako Lackson Tungaraza  (Lamax).

AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI.
@LACKSONTUNGARAZA
0764793105 - WhatsApp

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI