A-
Kwenye biashara kuna kukuru kakara nyingi sana. Unaweza Ukapoteza pesa zako
zote ulizoanzishia.
B-
Fursa yo yote Ile ina Hatari ya kupata HASARA kabla ya FAIDA, tofauti Ipo
kwenye Asilimia.
C-
Mradi/BIASHARA yenye FAIDA kubwa sana ina hatari/vikwazo Vikubwa pia. Na kama
FAIDA ni Ndogo, basi na hatari zake ni za kawaida. UNAWEZA UKAFUGA KUKU NA
WAKAFA WOTE AU KUIBIWA
Ndivyo
BIASHARA zilivyo.Matajiri wakubwa kama Donald Trump nao Walishakumbwa na hiyo
mikasa - kuna Kipindi aliwekeza na kufilisika kabisa.
Kwa
hiyo: "kabla ya kujiingiza kwenye biashara au FURSA, tathimini kama una
Uwezo wa kustahimili hasara yo yote Ile utakayoipata huko mbeleni." -
Lamax.
"USHUHUDA WANGU."
-
Nilipokuwa Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka wa Pili, nilipata WAZO la kuanza kuuza
viatu vya Kiume. Kwa hiyo nikachukua pea kadhaa za viatu Dar na kwenda navyo
chuoni, nikiamini ya kwamba Vitapendwa na kuuzika Fasta. Nilipofika nikaandaa
Tangazo na kubandika sehemu mbali mbali chuoni, na Pia Kusambaza kwenye Makundi
ya WhatsApp.
Baada
ya hapo nikaanza kusubiria Wateja. Mungu Sio Athumani, Wakaanza kuja, lakini
Kila kiatu wanachopima wanasema Hawapendi Rangi, Hawapendi Muundo, au Hakuna
vya Kuwatosha (Kwa maana ya size). Jambo hilo likawa linaniuma sana. Lakini
nikaendelea kuwa na Uvumilivu. Baada ya Muda vikanunuliwa viatu kadhaa na
vingine kubaki vikiwa vinanikodolea tu macho.
Baada
ya Kuona ya kwamba Vinanijazia tu nafasi Chumbani kwangu na haviuziki,
nikamtafuta jamaa niliyekuwa najuana naye, nikampatia hivyo viatu aviuze.
Wakati wa Likizo, Jamaa akavichukua viatu vyote na kwenda navyo nyumbani kwao
kijijini. Nilipomwuliza Baada ya Muda fulani, jamaa akaniambia Wadogo zake
walivichukua na kuvivaa. Hilo Jambo lilinikera sana ajabu. Lakini nikamwacha
nilipoona ya kwamba shida ilikuwa kwangu kwa kumwamini mtu asiyejua kuwa makini
na biashara. Kwahiyo nikapoteza zaidi ya laki moja.
"WATU
WENGI WANASHINDWA KUNUFAIKA KWENYE FURSA NA BIASHARA WANAZOZICHAGUA kwa Sababu
ya MIHEMUKO MINGI YA KUONA YA KWAMBA WATAFANIKIWA HARAKA HARAKA. Na hiyo yote
inatokana na MAHESABU YA KWENYE MAKARATASI."
Naamini
Kuna Jambo Zuri sana ulilojifunza hapa, basi Litendee Kazi. Na kama Unahitaji
Vitabu vyangu LACKSON TUNGARAZA usisite kuwasiliana nami moja kwa moja WhatsApp
kwa kubofya hii LINK: https://wa.me/255764793105 . UNAWEZA KUPATA VITABU VYA
HARD COPY (Nakala Ngumu) na SOFT COPY (Nakala Laini ya kusomea kwenye Simu au
Kompyuta yako.
By
Lackson Tungaraza.
@LACKSONTUNGARAZA.
AMUA
LEO KUWA WA TOFAUTI.
0 comments:
Post a Comment