Sunday, March 17, 2019


Yesu alizaliwa kwenye familia ya kawaida kabisa, akawa mwana wa Seremala aitwaye Yusufu. Mazingira aliyokulia hayakuwa na Intaneti, mitandao ya Simu, mitandao ya Kijamii kama Facebook, Twitter, Youtube, na Instagram. Wala hakukuwa na Google ya kumsaidia kupata taarifa za Watu Wengine waliofanikiwa kabla ya kuja kwake Duniani. Lakini pamoja na hayo Yote aliweza Kuupindua Ulimwengu na Kuacha alama Chanya inayoishi siku zote.

Hiyo ina maana ya kwamba, haijalishi tumezaliwa kwenye Familia ya aina gani - haijalishi Wazazi ni Wakulima, Wafugaji, Waajiriwa, Fundi gereji, Wafagia barabara, Wasafisha vyoo, Makondakta wa daladala, Watibua vyoo, Waalimu wa Chekechea, au hawana kazi maalumu za Kufanya. SUALA LA KUFANIKIWA au KUTOKUFANIKIWA LIKO MIKONONI MWETU.

Kama Yesu aliweza kufanya Makuu Licha ya kutoka kwenye familia na Mtaa wa kawaida sana, Wewe na Mimi tunashindwaje!!

Tunachopaswa kufanya ni "kuacha Kulalamika" au "Kumlalamikia Ye Yote Yule", na kuanza "Kuwajibikia maisha yetu" (to take Responsibility of our life) - kwa Sababu Kulalamika au Kuwalalamikia wengine hakutatupatia faida yo yote Ile. Ila Kuwajibikia maisha yetu kutatusaidia Kukua Kiroho, Kiakili, na kiwili (growing Up Spiritually, mentally, and physically).

Kingine tunachopaswa kufanya ni Kumwamini Yesu aliyekwisha kufanikiwa kabla Yetu kuliko Mtu Ye Yote Yule.  Yesu mwenyewe alisema ya kwamba, "Amin, amin, nawaambieni, YEYE ANIAMINIYE MIMI (Yesu), KAZI NIZIFANYAZO MIMI, YEYE NAYE ATAZIFANYA; naam, na KUBWA KULIKO HIZO ATAFANYA."

Kila kitu kiko Wazi Kwetu katika Karne hii kuliko wakati wo Wote ule. Tunayomitandao inayotusaidia kupata Elimu ya Cho chote kile tunachokitaka, na pia tunaye Mungu anayeishi ndani Yetu (Roho Mtakatifu). Kwa hiyo, TUSONGE MBELE, TUACHE KULALAMIKIA MAMBO AMBAYO HATUWEZI KUYABADILI - Hatuwezi Kubadili Wazazi Waliotuzaa, Mahali tulipozaliwa, na Ndugu zetu. ILA TUNAWEZA KUYABADILI MAZINGIRA YA SASA, PAMOJA NA HALI ZETU ZA KIMAISHA. It can be Done, it's just a matter of time (Inawezekana, ni Suala la Muda tu).


Mungu wa Mbinguni awe pamoja nasi, na atujalie kupendana kama naye anavyotupenda Sisi.
@LACKSONTUNGARAZA



0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI