Saturday, March 16, 2019


Hodi Hodi Uwanjani, Lamax Naingia,
Nimetoka Darasani, Mkononi na wangu Dia,
Nyumbani kwetu Msasani, Mbagala pa Kuzugia,
Ngoswe sio Diwani, Useme Kura Kazikimbia.

Watoto sikilizeni, Vijana nanyi pia,
Shuleni sio Ukweni, Useme Mke Utampitia,
Shuleni sio Ufukweni, Vimini Kutuvalia,
Ngoswe sio Diwani, Useme Kura Kazikimbia..

Notes zisomeni, Review na Google pia,
Uzembe Uacheni, Jengeni yenu Tabia,
Dunia Imesheheni, Vitabu na nyingi Bia,
Ngoswe sio Diwani, Useme Kura Kazikimbia.

Ushauri Nawapeni, Bure bila Kulipia,
Shuleni sio Baani, Mapenzi Kuyazamia,
Maisha hayana Utani, Kufeli Kutawajia,
Ngoswe sio Diwani, Useme Kura Kazikimbia.

Vijiweni Ondokeni, Hukumu Imekaribia,
Rudini Ibadani, Mungu Atawakumbatia,
Shetani yuko Njiani, Viburi Kuwapatia,
Mapenzi Yaacheni, Tamaa ni Dhambi pia,
Ngoswe sio Diwani, Useme Kura Kazikimbia.

Waalimu wako Darasani, Mazuri kukupatia,
Njoo na Yako Wani, Zawadi Kujitwalia
Ngoswe sio Diwani, Useme Kura Kazikimbia.

SHAIRI hili la ‘NGOSWE SIO DIWANI’ limeletwa kwenu na LACKSON TUNGARAZA kwa Udhamini wa LAMAX QUOTES na Kitabu cha ‘SITARUDI NYUMA TENA’

@LACKSONTUNGARAZA


Related Posts:

  • ANDIKA JINA LAKO VIZURI Heri Kuchagua Jina jema kuliko Mali nyingi [smart phones, kompyuta, iPhone, iPad, gari, nyumba, nguo, shamba, ng'ombe]; Na Neema kuliko fedha na dhahabu.. Mith 22:1 Watu wengi sana hawajali juu ya majina wanayojiita au … Read More
  • WHAT DO YOU WANT TO BE REMEMBERED FOR?  Kwa kawaida kila mtu huwa anatamani na anapenda ya kwamba akitenda jambo, baadae Akumbukwe kwalo. Ikiwezekana hata watu kadhaa watoe shuhuda za jambo hilo. This a human character. Unataka kukumbukwa kwa lipi… Read More
  • "I DON'T STOP WHEN I'M TIRED, I STOP WHEN I'M DONE"*Akasema, YOTE IMEKWISHA. LIFE is PERFORMANCE. Na Mara unapoanza Kuperfom ndipo unaanza kutambua aina ya wasikilizaji na watazamaji ulionao. Aidha wako pamoja nawe, au la. That's how life is in this world. Bahati Bukuku a… Read More
  • FACEBOOK VS BLOG KIPI NI BORA KWA BIASHARA YAKO? Kumekuwa na sitofahamu juu ya namna ya kutumia mitandao hii katika kukuza biashara. Ndiyo maana nimekuuliza; Kati ya Facebook na Blog, ni kipi bora kwa Biashara yako? Jibu lako litaash… Read More
  • JE UNAJIKUBALI...! #KUJIKUBALI NI HATUA KUBWA SANA NA YA KWANZA KATIKA MAISHA ILI MTU AWEZE KUFURAHIA UUMBAJI WA MUNGU. #Hivi unamkubali kwa asilimia ngapi huyo unayemwona kwenye Kioo unapojiangalia? #Kuna waliojikatia tamaa kabisa, hawata… Read More

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI