Wednesday, August 8, 2018


Daudi kuwa porini na kuchunga kondoo kwa muda mrefu SI KWAMBA MUNGU ALIMWACHA AU ALIMSAHAU, maana ndugu zake hawakumhesabia thamani, mzee Yese alimtoa mawazoni mwake, hata anapo ambiwa alete watoto wake mbele ya nabii SAMWELI, utaona anawaleta watoto wake wote na hadi anapoulizwa tena je! "hakuna mwingine" ndipo anapokumbuka kuwa yupo Daudi porini huko, Yese hakumfikiria kama ndiye anayeweza pakwa mafuta, hakumfikiria kuwa ndiye MUNGU anayeweza kumchagua.


Mpendwa ngoja nikukumbushe jambo kwamba ndugu zako wanaweza kukusahau, familia yako inaweza kukupeleka machungani, wazazi wako wanaweza kukusahau, LAKINI SI MUNGU ALIYE KUUMBA KWA SURA NA KWA MFANO WAKE, huko huko uliko utafuatwa na kupakwa mafuta yakuwa mfalme, huko huko uliko utafuatwa ili upate kukaa katika nafasi yako, MAANA WANADAMU WANAWEZA KUSAHAU UWEPO WAKO, LAKINI MUNGU HAWEZI SAHAU HATA SIKU MOJA.


Tambua kwamba huko machungani uliko MUNGU amekuweka huko kwa ajili ya mafunzo maalumu, atakupambanisha na SIMBA, atakupambanisha na DUBU, kwasababu anaijua kazi iliyopo mbele yako, Anajua kwamba kunajamaa ANAITWA GOLIATHI itakupasa upambane naye, huwezi pambana na GOLIATHI kama hauna uzoefu maana GOLIATHI ni mzoefu wa vita.


Tambua kwamba hayo unayopitia unapitia kwasababu tu, MUNGU anaijua kazi iliyoko mbele yako ni lazima upitie huko kwanza, vita iliyopo mbele yako ni kubwa kuliko unayopigana sasa, ukishinda vita ya wakati huu, ukiwauwa hao simba na dubu, HATA GOLIATHI AKIJA Amini HAITAKUWA SHIDA KWAKO KUMUANGAMIZA.


NI MAOMBI YANGU MUNGU AKAPATE KUSEMA NA WEWE KATIKA KILA KIPINDI UNACHOPITIA, NA NI MUHIMU UTAMBUE KUWA UPO DARASANI KATIKA HAYO UNAYOPITIA. KWA HIYO USIPITE BILA KUJIFUNZA KITU, KUWA TAYARI KUFUNDISHIKA KATIKA YOTE UNAYO PITIA.

Related Posts:

  • HATA WANADAMU WAKIKUSAHAU, MUNGU BADO ANAKUKUMBUKA Daudi kuwa porini na kuchunga kondoo kwa muda mrefu SI KWAMBA MUNGU ALIMWACHA AU ALIMSAHAU, maana ndugu zake hawakumhesabia thamani, mzee Yese alimtoa mawazoni mwake, hata anapo ambiwa alete watoto wake mbele ya nabii SAM… Read More
  • JE UNAOGOPA KUPINGWA? Leo ukimwuliza Mtoto wa Darasa la Kwanza 1-5 (Moja kutoa Tano) ni Sawa sawa na ngapi, atakwambia haiwezekani, ni Lazima pawepo mahali pa kukopa. Lakini ukimwuliza hilo hilo Swali aliye Darasa la Tano atakwambia ni Sawa sawa… Read More
  • NGOSWE SIO DIWANI, USEME KURA KAZIKIMBIA. Hodi Hodi Uwanjani, Lamax Naingia, Nimetoka Darasani, Mkononi na wangu Dia, Nyumbani kwetu Msasani, Mbagala pa Kuzugia, Ngoswe sio Diwani, Useme Kura Kazikimbia. Watoto sikilizeni, Vijana nanyi pia, Shuleni sio Ukwen… Read More
  • NAMNA AMBAVYO WATU WENGI NI WAFUNGWAWatu wengi hawataki kuwa huru kabisa.  Watu wengi hawataki kuachana na UTUMWA. Wakiambiwa, hawaamini, na Kudhani ya kwamba wanafatiliwa maisha yao. Kati ya mambo yaliyomtia hamasa Mwalimu  Nyerere kuacha Ualim… Read More
  • KWAKO KIPENZI CHANGUNinayaandika haya nikiwa na majuto makubwa sana ndani yangu, kiasi cha Kuona ya kwamba dunia nzima inafahamu historia yangu. Sikutaka kuyaandika haya, ila sipendi uendelee kuteseka kwa sababu yangu. Licha ya kwamba kwa sas… Read More

0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI