Heri
Kuchagua Jina jema kuliko Mali nyingi
[smart phones, kompyuta, iPhone, iPad, gari, nyumba, nguo, shamba, ng'ombe]; Na Neema kuliko fedha na
dhahabu..
Mith 22:1
Watu
wengi sana hawajali juu ya majina wanayojiita au wanayoitwa [mwendokasi, msiba,
playboy, muuza sura, kikaango, taabu, huzuni] .. Badala yake wanajali Mali
nyingi(magari, nyumba, mashamba) pamoja na fedha na dhahabu.
Wako
tayari kucheza uchi mbele ya Kamera[mfano video ya chura, diamond] na hata
kuvaa mavazi ya kuonesha maungo ya ndani ili tu wapate Mali nyingi pamoja na
fedha.
Wako
tayari kutembea wa waalimu wao, wazazi wao, waajiri wao, wachungaji wao ili
watengeneze Mali nyingi. Wanasahau ya kwamba HERI KUCHAGUA JINA JEMA KULIKO
MALI NYINGI.
Kunamuunganiko
kati ya historia ya Mtu na Jina lake. Unaitwa Malaya, shoga, playboy, mzinzi,
kahaba, changudoa... Unadhani historia yako itakuwaje? Kuna watu ambao hata
kufariki kwao jamii ilisema *Afadhari Mtoto wa fulani kaondoka duniani maana
alikuwa kero hapa mtaani.. Kila binti ni mimba, wake za watu kuwaonga* Historia
hujengwa kuanzia katika Jina ulilochagua.
Neema
kuliko fedha na dhahabu. Neema inayoongelewa hapo ni neno la Kristo. Neno la
Mungu ni zaidi ya fedha na dhahabu... Ukipokea neno umepokea vyote. Uko tayari
kuandikiwa Historia njema? Chagua Neema pamoja na Jina jema... Mungu Vs Kusudi.
Jina
linabeba maana na Kusudi.
Yesu
maana yake ni Mkombozi, Kusudi ni Kukomboa watu wake na dhambi zao #Mathayo
1;21.
Jina
lako linamaana na Kusudi gani?
Acha
kutembea na wanawake wanaokuzidi umri almaarufu kama mashugamami ili upate Mali
nyingi au fedha. Acha kuchanganya wanaume ili upate fedha... CHAGUA NEEMA
KULIKO FEDHA NA DHAHABU. JINA JEMA KULIKO MALI NYINGI.
Now
Is Your Time to Choose a better name and Grace. Mwl. Emmanuel Makwaya Godfrey
anasema To Be Is To Do, Shemeji Melayeki anasema From Reading to Leading,
Pastor Raphael Joachim Lyela anasema Kama unabisha Ogelea kwenye Gundi.
Proudly
sponsored by
N.Y.I
MOVEMENT
*Join
today and Be part of the Change*
©Lackson
TungarĂ za
0764793105
whatsapp/call°
www.facebook.com/ltungaraza [Facebook]
0 comments:
Post a Comment