Palikuwa na
familia iliyokuwa na binti mrembo ambaye alikuwa bado hajaolewa na makazi yao
yalikuwa mlimani, nje ya mji. Vijana wengi walitamani sana kumwoa huyo binti,
hivyo wazazi wa binti wakatangaza ya kwamba mtu atakayeweza kufika huko
kilimani basi atapata nafasi ya kumwoa binti yao.
Kijana mmoja
akajitolea na kuanza safari ya kuelekea huko mlimani, akiwa njiani alikutana na
mzee mmoja aliyemjulisha ya kwamba haimpasi kuendelea na safari yake kwani njia
siyo salama… mbele kuna sauti nyingi za watu za kutisha, zikisema *Huyooo,
huyoooo, huyooo* kama mtu anayezomewa na kadri unavyozidi kusogelea kilima
ndivyo na kelele hizo huongezeka, kiasi cha kusema *mkamate huyo tumwue, awe
kitoweo leo* lakini usitazame nyuma wala pembeni hata kama ukisikia hiyo sauti
ikisema karibu nawe maana utakuwa Jiwe papo hapo.
Kijana akaondoka
na kujisemea ya kwamba hiyo ni kazi ndogo kwake. Alipofika mbele ya safari,
kadri alivyosogelea kilima hicho na ndivyo sauti za kumkamata na kumwua zilivyoongezeka…
uvumilivu ukamshinda na akaamua kuangalia ni nini, hapo hapo akawa Jiwe kama
yule mzee alivyomwambia.
Vijana wa aina
mbali mbali walijaribu na wote wakawa mawe… mlima ulijaa mawe mengi yaliyokuwa
watu. Kijana mmoja mdogo mdogo tu naye akajitolea kwenda. Yule mzee alivyomwona
alimhurumia sana na kumwambia arudi tu nyumbani kwao maana yeye bado ni mdogo
sana, isitoshe watu wengi washakuwa Mawe kwa sababu ya kuangalia pembeni na
nyuma waliposikia sauti za kuzomewa na kuuawa. Kijana hakujali hilo, akaanza
safari hiyo na kuelekea mlimani. Njiani aliyaona Mawe hayo, akasikia sauti
nyingi nyuma na pembeni zikisema “huyooo, huyooo, mkamate.” Hakujali, akaendelea
na safari. Alipokaribia kufika akasikia wakisema “mkamate huyo huyo tumchinje
n.k.”
Kijana akaweza
kufika licha ya vitisho hivyo vyote… akamwoa yule binti mrembo. Dawa ikatafutwa
na yule binti, na wale waliogeuka mawe wakabadilishwa na kuwa watu tena.
Nini unajifunza hapa….
Katika maisha
utakutana na kila aina ya maneno na matendo, pale utakapokuwa ukitaka kufanya
jambo kubwa la kimaendeleo. Utazomeewa, utatishwa, utaogopeshwa, Utaambiwa ya
kwamba hutoweza kwa sababu wengi washajaribu na kushindwa, utasengenywa,
kutemewa mate, kukataliwa n.k… Uamuzi ni wako, uendelee mbele kama huyo Kijana
aliyeamua kutokuangalia pembeni wala nyuma na kumwoa binti mrembo, au uwatazame
na kuwa Jiwe {mtu asiye na mafanikio, wa hali ya chini, wa kawaida sana}.
Nabii Musa
aliamua kutoka katika nyumba ya Farao, ya kifalme licha ya maisha mazuri
aliyopewa na kufundishwa hekima yote ya Wamisri. Najua yalisemwa mengi, lakini
hakujali hayo… Leo ni mmoja wa Manabii wakubwa katika historia ambao walikuwa
mashujaa kweli kweli.
Mwanamke yule
aliyetokwa na damu kwa muda wa miaka 12, kuangaika kwa mikono ya matabibu wengi
na asipate tiba. Hakujali ya kwamba watu watasema, watamwonaje, watamchukuliaje…
Alipenya kati ya umati wa watu wengi na kugusa Pindo la vazi la Yesu Kristo na
mara hiyo hiyo damu yake ikakoma na kuwa mzima kabisa.
Be concentrated, and let no one pull you out of the way to prosperity.
“When you’re in the light everything follows you,
when you enter into the darkness, even your own shadow doesn’t follow you” –Adolf
Hitler.
God knows you well, and He loves you
automatically. Worship, trust and follow Him completely, and your life will no
longer be the same forever.
Unaweza pia
kunipata katika maeneo yafuatayo kwa ukaribu;
Twitter: @lacksonthecoach
Instagram: LACKSONTUNGARAZA
WhatsApp/sms: 0764793105
TWENTY YEARS TO COME BEGINS TODAY, MAKE EVERY MINUTE COUNTABLE.
WASTE NOT YOUR TIME
Maoni yako ni ya muhimu sana hapa. Karibu
ReplyDelete