Proudly Sponsored by
N.Y.I
MOVEMENT
*Join and Be
part of the Change*.
Kuna mambo
mbali mbali ambayo wewe kama Kijana mwenzangu unaweza fanya pasipokuwa na pesa
kubwa Bali hiyo hiyo uliyonayo hapo .... Akili, maarifa, elimu, ujuzi ni Mitaji
pia.... Kwanini bado unalalamika ya kwamba maisha siyo mazuri? Badili sasa
mtazamo wako, waliofanikiwa maishani ni watu waliyogundua ya kwamba Mtaji siyo
pesa pekee Bali pia uwezo ambao Mungu kakuumbia ndani yako.
Watu kama
akina Ronaldinho Gaucho, Barhesa siyo kwamba walikuwa na pesa nyingi pindi
wanaanza safari ya kusaka life.. Waliamini ya kwamba kuna zaidi ya Pesa ndani
yao. Ni sawa na kuacha migodi Ya dhahabu Tanzania na kwenda kutafuta dhahabu
Somalia..
Huo ni upuuzi. What's your talent, experience,
profession, hobby? Then why do you complain about having a hard life? Be a
critical Thinker....
Wewe ni
zaidi ya Unavyojitazama... Unamadini ndani yako..... Mwandiko wako ni wa
kipekee duniani, mboni ya macho yako ni ya kipekee, nyayo za miguu yako ni ya
kipekee, alama za mikono yako ni ya kipekee... So what next? You
have greatness within you... Use it.
Lackson Tungaraza
www.lacksontungaraza.blogspot.com
Nabii Musa
kipindi amefika na wana wa Israeli katika kando ya bahari ya shamu... Watu
walianza kumlilia Musa kwa kuwaleta kufa kifo cha aibu na pia Musa akaanza
kumlilia Mungu atende jambo... Unajua Mungu alimwambiaje Musa?.... Usinililie,
Chukua fimbo yako uinyooshe juu ya bahari... Aliponyoosha, bahari ikawa nchi kavu
nao wakapita saa hiyo. Musa alikuwa na Mtaji wa kusogea mbele mkononi mwake
lakini hakutambua.
MTAJI SIYO PESA TU, TUMIA UBONGO WAKO VYEMA KUFIKIRI VIZURI. |
Ni wakati wa
akili za watanzania kufunguka na kuwa wazi..... Bado hujaelewa tu ?.... Iko
hivi…
Kuna
shughuli unaweza Fanya hata kama hauna pesa na ukatengeneza bomba la Pesa....
Unaweza kuwa
Mshauri wa mambo ya biashara: Wewe una
uzoefu wa ujasiriamali au umiliki wa biashara? Unajua nini kinahitajika ili uanzishe
biashara, kujenga biashara, kuongeza biashara na kukua? Sasa unaweza kuanza
kazi ya ushauri wa biashara. Unaweza kusaidia kampuni au biashara mbalimbali
kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo muhimu. Unaweza
kuwasaidia watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na kuingia kwenye
ujasiriamali kwa malipo.
Hujaelewa
tu!! amka wewe.
wewe kama Kijana mwenzangu, unawaza nini juu ya MTAJI? Toa maoni yako hapa
ReplyDeletewewe kama Kijana mwenzangu, unawaza nini juu ya MTAJI? Toa maoni yako hapa
ReplyDelete