Kila mara watu tunajikuta tupo au tunaingia wenyewe katika
Mazungumzo, na hayo mazungumzo yanaweza yakawa yenye kuleta Matokeo chanya au
hasi. Hivyo uhalali wa matokeo ya mazungumzo unategemeana na wahusika binafsi.
Leo katika harakati zangu za kila siku kama Mungu
anavyonijalia, nimeweza kupata nafasi ya kuhojiana na Kijana mmoja[Joseph Fande]
aliyenitumia Meseji asubuhi kabisa na nilivyotoka Ibadani maongezi yakawa kama
ifuatavyo;
Joseph
Fande: Kaka naomba kujiunga na kundi lako naitwa Joseph
Fande nina miaka 21 natokea Dodoma, nahitaji kufanya biashara ila Mtaji sina,
nifanyeje nipo tayari kufanya utakachonielekeza na kukitekeleza mara moja,
nisaidie Lackson Tungaraza.
Lackson
Tungaraza: Mimi Lackson Tungaraza.. Namba yako ya wasap ni
ipi?
Joseph:
simu yangu haina Whatsapp, ina facebook tu
Lackson:
si umesema nikuunge kwenye kundi langu au..
Joseph:
Yaani nahitaji kitu ulichokizungumzia kuhusu Niwe na Pesa
Lackson:
Uko sehemu gani?
Joseph:
Dodoma, wilaya Kongwa, kijiji Ibwaga
Lackson:
unajishughulisha na nini ndugu…
Joseph:
Ni mkulima na ila kipindi cha kiangazi nafanya kazi ya udalali, mtu anaweza
akanipa ela yake nimnunulie mazao
Lackson:
unafamilia au… yaani unamke na watoto..
Joseph:
Ee lakini siishi nae
Lackson:
kupitia haya maswali nitapata kukushauri.. usishangae
Joseph:
Aya
Lackson:
Pesa ambazo huwa unapata kama faida umezifanyia kitu gani hadi sasa..
Joseph:
Huwa nanunua kuku wa kufuga
Lackson:
umeshawafuga wengi..
Joseph:
Aa so wengi sana
Lackson:
chagua kufuga kwa biashara au chakula
Joseph:
kwa biashara
Lackson:
katika maisha ili ufanikiwe, inabidi uchague jambo moja ambalo ndilo utaliwekea
nguvu kubwa, ndipo mengine madogo madogo baadae
Joseph:
sawa
Lackson:
Barhesa anavitega uchumi vingi lakini anasifika kwa kupitia AZAM COMPANY
kwasababu ndipo nguvu yake kubwa alipoielekeza.
Lackson:
Baada ya kuona Kampuni ni kubwa, akafungua na mifereji mingine ya pesa ya
kuendelea kuhudumia kiwanda chake
Lackson:
Ni jambo gani/kipaji gani ambacho unajivunia kuwanacho au jambo gani ambalo
unapenda kulifanya kutoka moyoni na kila mara unapata hamasa ya kulifanya hata
kama wengine hawalithamini kwa sasa? [hata wewe msomaji, unaweza kujiuliza hili
swali]
Joseph:
Yaani jambo nililopanga kulifanya katika maisha yangu niwe na Duka na Mashamba
Lackson:
Ndilo jambo linalokuangaisha moyoni usiku na mchana ya kwamba ni wewe ndiwe
uwezayekulifanya vizuri zaidi ya wengine?[Fikiria na wewe msomaji]
Joseph:
Maana jambo lenyewe niliwahi kulifanya kwahiyo ndo maana nataka sana kufanya
Lackson:
Ikiwa ndilo unalopenda kufanya kuanzia moyoni, utafanikiwa kwa hakika. Upendo
unanguvu kubwa kuliko tamaa. Baada ya kuwa umepata jambo ambalo unahitaji
kulifanya ili kubadilisha historia ya maisha yako.. Weka malengo, baada ya muda
Fulani unataka uwe umefika katika viwango gani. Malengo ya mwaka, miezi, mwezi,
wiki hadi siku na masaa. Kila siku unafanya jambo ambalo linakupa nafasi ya
kusogelea Malengo yako ndani ya Ndoto uliyonayo.
Think Big, start small…
Fikiri kwa mapana, kubali kuanza kidogo. Mbuyu ulianza kama mchicha, mbegu ya
haradali ni ndogo kuliko zote lakini hukua na kuwa mmea mkubwa kuliko mingine.
Joseph:
Aha unaushauri mzuri kaka, ntaufanyia kazi
Lackson:
Amini pande mbili katika maisha… Moja ni MUNGU pekee na wa Pili ni wewe pekee.
Wanadamu wanaweza badilika lakini Mungu habadiliki, wanaweza kukuhukumu kwa
vile hawajui unapotaka kufika, na hata kukutenga… Mungu yupo nawe, labda
umwache wewe.
Jitahidi kuwa Mwaminifu sana kwa wale wote
unaowahudumia… Mteja mmoja, huleta wateja wengine. Watu waaminifu ni adimu
karne hii, ukiwa hivyo utawavuta wengi kuja kufanya kazi nawe… hata mimi
napenda kufanya kazi na waaminifu.
Mafanikio yanagharama yake… Muda, Maarifa na Pesa.
Tumia Muda wako katika kufanya mambo yanayoendana na Ndoto yako hiyo, tafuta
Maarifa ya kuifanya Ndoto yako iwe na nguvu kama kusoma vitabu sahihi na
kuhudhuria Semina mbali mbali, na Pesa kuihudumia Ndoto yako.
Joseph:
Nakushukuru sana kaka yangu kwa ushauri wako
Lackson:
Swali uliza
Joseph:
Mpaka hapa sina la kukuuliza kaka ahsante
Lackson:
Kuwa na Nidhamu ya Pesa… Usitumie fedha katika mambo yasiyo ya lazima
kama ulevi, kuonga, starehe n.k..Pesa unayopata ya faida, iweke kwenye Duka na
Mashamba kama ulivyosema unataka uwenavyo. Amini unaweza, amini utafika siku
moja kwa kuendelea kufanya kuanzia sasa
Joseph:
Mungu akubariki.
Hayo ni mazungumzo kati yangu na Kijana Joseph
Fande, ili upate kuelewa vyema hili somo ni kujichukulia ya kwamba wewe ndiwe
Joseph Fande na maswali niliyomuuliza huyajibu wewe.
Ikiwa unajambo lolote la kunishirikisha, karibu sana
mlango uko wazi siku zote.
WhatsApp: 0764793105
Facebook: www.facebook.com/ltungaraza [Niunge
niwe rafiki yako, uzidi kupata masomo haya kwa ukaribu zaidi]. Ahsante sana na
uwe na baraka za Mungu milele.
Baada ya Screenshots za Mazungumzo yetu;
0 comments:
Post a Comment