Moja ya tafsiri za
Maisha nilizowahi kuzisoma na kuzisikia ni kwamba Maisha ni Mbio. Cha
kujiuliza, “Unakimbizana na nani?” Nimegundua ya kwamba Maisha ni Mbio ambayo
Mshindani ni wewe mwenyewe… unajipulizia mwenyewe kipenga/firimbi na kuanza
kukimbia kwa kushindana na wewe mwenyewe. Mtu atajiuliza, “ninawezaje
kujikimbiza mwenyewe au kushindana na mimi huyo huyo ninayekimbia!!?” Nami
nikuulize Swali jepesi, “Ukiwa peku na ukawa unachomwa na misumari, utafanya
nini?” Najua ya kwamba utatafuta suluhisho la tatizo hilo, unaweza ondoka hilo
eneo au ukanunua viatu ambalo ndiyo linaweza kuwa suluhisho bora kuliko la
kuondoka eneo hilo kwa sababu unaweza kukutana na tatizo hilo hilo katika eneo
jingine.
KIMBIA... USICHOKE... USITAZAME NYUMA... |
Maisha ni Mbio, Mshindani
ni wewe mwenyewe… shindana na huyo unayemwona katika kioo unapojitazama. Kama
yeye hajavaa tai mwambie ya kwamba wewe unaenda kuvaa tai, kama yeye ni mpenda
starehe mwambie ya kwamba wewe unaacha starehe za hovyo hovyo na kutumia hiyo
pesa katika uwekezaji kwenye vitega uchumi mbali mbali… tamani kuwa zaidi ya
huyo unayemwona katika Kioo unapojitazama.
Nimefatilia kwa kiasi
Fulani juu ya mashindano ya mbio alimarufu kama Marathon Race. Nimegundua
ya kwamba wanapoanza kukimbia huwa hawatazami ni nani anayekuja nyuma yao, bali
ni nani aliyeko mbele yao pamoja na mstari wa kumalizia mbio (Finishng Line).
Nilipokuwa katika shule
ya msingi, nilikuwa nikishuhudia rafiki zangu wengi wakianguka katika Mbio na
kuumia kwa sababu Ya kuangalia nyuma kuona wanaowakaribia. Binadamu
unapokimbia, ni tofauti na gari… gari linavioo vya kumwezesha dereva aone
anayemfuata kwa nyuma. Binadamu unapoacha kutazama aliyepo mbele yako na Finishing Line na kuanza kutazama nyuma,
utapoteza dira ya mbele na kuanguka ama kupoteza katika huo mchezo.
Nimekuandikia haya siku
hii ya leo kwasababu mimi binafsi Lackson Tungaraza nimeona madhara yake. Watu
wanaacha kutia bidii katika maisha yao na kuanza kuangalia yaw engine ya kwamba
ni bora kuliko ya kwao.
Ngugu yangu, jifunze
leo kuachilia yale uliyoyapitia katika Maisha na kutia juhudi katika yale
yanayokuja mbeleni. Usimalize muda wako mwingi unawaza juu ya hasara ya mwaka
uliyopita katika biashara, juu ya mchumba aliyekudanganya, juu ya magonjwa
yaliyokupata, juu ya masomo uliyofeli mwezi uliyopita, juu ya watu wanaokusema
kwa ubaya… huo muda utumie katika maandalizi ya vita inayokuja mbele yako,
yaliyopita yawe ni silaha ya kushinda yale yajayo.
Washinde wale waliyoko
mbele yako wanaokuzuia kufikia Finishing Line na kuwa wa kwanza katika Mbio…
wale wanaokukatisha tamaa na kukwambia ya kwamba hautofanikiwa kwa sababu wengi
wameshajaribu na kushindwa, wale wanaokwambia ya kwamba ule Ujana maisha yapo
tu, wale wanaokwambia kuwa na wapenzi wengi na kufanya Uasherati/Uzinzi ndiyo
ujanja… Refuse to be part of destruction, but part of construction.
Usisubiri hadi mtu
akupigie firimbi ndipo ukimbie, puliza wewe mwenyewe kuania sasa. Maisha ni
wewe, siyo yeye au wao au sisi.. ndiyo maana Mungu anamtafuta mtu wa kuitenda
kazi yake na siyo watu. Be Responsible for your future, Be Responsible for
the Race.
Wasambazie na rafiki
zako ujumbe huu WhatsApp, Facebook, Twiiter na katika mitandao mbali mbali ya
kijamii ili nao waweze kuwa sambamba na maisha…. Karibu pia katika kundi langu
la Whatsapp [0764793105]. Uwe na wakati mwema, tukutane tena katika mada
nyingine….toa maoni yako kwa mada yoyote ile ambayo unatamani niigusie zaidi
ambayo nimekwisha kuifundisha lakini haikuelewa au bado sijaifundisha na
unaipenda, karibu sana usisite kwasababu ndiyo mwanzo wa Kukimbia kwa Staili
nzuri.
0 comments:
Post a Comment