Ni nini maana ya neno
‘Maisha?’
Kila mtu anaweza kutoa
maana ya neno Maisha kwa yale aliyoyapitia, anayoyapitia au anayotarajia
kukutana nayo mbeleni. Maisha yanamaana nyingi sana na kulingana na mtazamo wa
kila mtu, jaribu kujiuliza wewe binafsi, maisha yanamaana gani kwako. Je, kuwa
na Mke Mrembo ndiyo maisha? Kuwa na Magari na Majumba ya Kifahari ndiyo Maisha?
Nimesikia watu wengi sana wa Vijijini wakisema ya kwamba wanaenda Mijini
kutafuta Maisha, sijui maana ya Maisha kwao ni nini hadi wanaenda kuyatafuta
Mijini na siyo Vijijini.
Hiyo yote ni mitazamo
kama nilivyosema hapo awali, naomba leo Lackson Tungaraza nizungumzie Maisha
kwa namna ambayo mtu anakuwa Kimwili na Kiakili. Ukujitazama hapo ulipo sasa na
jinsi ulivyokuwa Miaka miwili au mitatu huko nyuma ni tofauti kabisa; Aidha ni
kiumbile au kiakili. Kama vile ambavyo imekuchukua muda mrefu kufikia kimo cha
urefu ulionao leo na uwezo wako wa kuchukulia mambo kwa upana zaidi, ndivyo
ambavyo nasema MAISHA NI HATUA… Mlolongo wa Mambo.
Mafanikio pia katika maisha ni hatua, hakuna Mafanikio ya kulala Maskini na
kuamka Tajiri hata kama ni kwa kutumia nguvu za giza au kuwa mwanachama wa
Freemasons kama wengine wanavyodhani… bado kuna mambo kadha wa kadha
yanakuhitaji kutenda kwanza ili kufika kule unakotaka. Mambo mazuri
hayapatikani haraka au kwa uwepesi, dhahabu ni ya thamani sana na ndiyo maana
hata upatikanaji na uchimbaji wake ni mgumu.
Kuna watu ambao
wamekata tamaa kwa sababu yay ale waliyoyapitia au wanayoyapitia sasa… Rafiki
na ndugu wamewatenga kwa sababu ya umaskini wao, waume wao wamewaacha kwa
sababu wanaonekana ni kama Magoli kipa… Ni waambie tu ya Kwamba Life Is A Process
as long as you want to grow.
Chukua maamuzi leo ya
kuwa dereva wa maisha yako na uangalie ni barabara gani nzuri utakayotumia ili
safari yako iwe salama. Najua kuna mambo mengi ambayo unatamani uwe nayo kwenye
maisha, hayatakuja hadi uyatafute… Atafutaye huona, abishaye hufunguliwa,
aombaye hupewa. Anza kufanya hatua kwa hatua bila kuogopa changamoto ukiamini
ya kwamba siku moja mambo yatakuwa sawa maana unamtumaini Mungu… One day YES,
by doing not saying. Mtoto mdogo anapotaka kutembea, hata
akianguka mara ngapi na kuumia bado anaendelea tu kujaribu tena na tena hadi
atembee. Wakati mwingine Mama yake anamnunulia kigari kidogo cha kujifunzia
kutembea, nawe ikiwezekana tafuta mtu au watu ambao watakusaidia kusonga mbele.
Siku moja waliokuwa
wanakucheka na kudharau juhudi zako, watakusalimia kwa heshima na kuomba Siri
ya Mafanikio yako. Chukulia mfano wa mti unapokuwa mdogo (Mche) watu
huwa wanaudharau na hata kuupiga piga mateke na kutegea katika kuupatia maji ya
kutosha. Lakini pindi unapokuwa mkubwa, wale wale watu hutafuta kivuli kwenye
huo Mti, kupata Mbao kwaajili ya Ujenzi na wengine kupata dawa pamoja na
vitamin C kwa maa ya Matunda. You Present Situation is not final destination,
the Best is yet to come.
MAISHA NI MFANO WA MCHE UNAOKUA |
Tazama Changamoto kama
ni daraja la kukuvusha kwenda ng’ambo ya pili… ANegative Thinker sees a Difficulty
in every Opportunity while a Positive Thinker sees an Opportunity in every
Difficulty… The word NO means Next Opportunity. Bila Changamoto
nilizopitia katika maisha, nisingekuwa na uwezo wa kuandika haya unayoyasoma
hivi leo wala kugundua ya kwamba Kalamu ya Uandishi ndiyo Silaha yangu ya
kuifikia jamii. Ndiyo maana sahivi nachukulia Changamoto kama Ngazi ya
kunipandisha juu… huwezi kuwa mtu mkubwa maishani bila kupitia mambo makubwa,
angalia maisha ya Mfalme Daudi au Mwl. Nyerere ndipo utaelewa ninachokiandika
hapa… I have Never met a great person with an Easy past.
Natumaini ya kwamba
utakuwa umepata Maarifa ya kukusaidia kusonga mbele zaidi kwa sababu Life Is A
Process… Hutaogopa tena Changamoto wala kuwa na hofu ya kuonesha thamani yako
katika jamii… Wasambazie na rafiki zako ujumbe huu WhatsApp, Facebook, Twiiter
na katika mitandao mbali mbali ya kijamii ili nao waweze kuwa sambamba na
maisha…. Karibu pia katika kundi langu la Whatsapp [0764793105]. Uwe na wakati
mwema, tukutane tena katika mada nyingine….toa maoni yako kwa mada yoyote ile
ambayo unatamani niigusie zaidi ambayo nimekwisha kuifundisha lakini haikuelewa
au bado sijaifundisha na unaipenda, karibu sana usisite kwasababu ndiyo mwanzo
wa Life Is a Process.
0 comments:
Post a Comment