~Nilipokuwa mtoto nilipendelea sana kutazama muvi za
ngumi ( action movies), katika kuangalia kwangu nilishangaa kuona ya kwamba
muhusika mkuu wa Muvi ambaye ndiye anaitwa STARRING alikuwa hafi hata kama
amekutana na majanga kiasi gani.
~ Wanajeshi wengi walikuwa wanaagizwa kwenda
kukomboa mateka Vietnam, wengi walikuwa wanauawa sana tena kinyama lakini
STARRING alibaki kuwa hai. Japokuwa alikuwa anapigwa kisawa sawa hata kulko
wanajeshi wenzake lakini bado alibaki kuwa hai na kushinda vita.
~KWANINI UWE STARRING WA MAISHA YAKO? Inawezekana
umesoma kichwa cha somo na hukuelewa au ulitafsiri kivingne. Starring siku zote
ndiye Muhusika mkuu wa fedha na ndiye mwamuzi wa mwisho wa hatima ya Adui zake
ambao ndiyo huitwa Majambazi au Mamluki.
~Ili ufanikiwe maishani mwako kwa jambo lolote lile
kuanzia sasa unaposoma ujumbe huu wa Lackson Tungaraza, jaribu nafasi ya kuwa
STARRING wa maisha yako. Acha nafasi zingne zote za uigizaji kama Ulinzi, Ubaba
au Umama..kuwa Starring. Changamoto zisikukatishe tamaa ya kuendelea mbele.
Majungu ya watu yasikurudishe nyuma kabisa. Wewe ni Starring na mwisho wa picha
wewe ndye Mshindi.
~Sijawahi ona jambazi ndiye anakuwa mshindi wa
Muvi..ikiwa hivyo basi ujue kuna mwendelezo wa hiyo Picha(new episode). Ni
maamuzi yako juu ya hatima ya Yale yanayokukumba katika maisha ya kila siku.
Kama movie ambavyo jambazi akibaki hai hadi mwisho wa picha wanatengeneza
mwendelezo wake...hunabudi na wewe kusimama tena na kurudi kupambana hata kama
mwanzoni ulikuwa umekata tamaa katika biashara, masomo au ndoa yako. Katika
episode inayofuata jihakikishie wewe Starring kuwa Mshindi bila kufa.
~ Mimi nimeshachagua kuwa STARRING wa maisha yangu.
Ndiye mwamuzi wa hatima ya changamoto zinazonikabili(jambazi katika muvi)...
Simlaumu mwingne ila ninapambana nazo kwa kutumia maarifa mbalmbal ya
kiuStarring. WEWE JE? Hujachelewa, amua sasa . THE DOOR TO SUCCESS IS OPEN,
WAITING FOR YOU TO ENTER. Make a move.
~ Natumaini umejifunza jambo litakalokusaidia
maishani. Sambaza kwa wengne pia wapate maarifa bila kuedit chochote na
utabarikiwa sana. Usisite pia kutoa maoni yako.
By Lackson
Tungaraza
0764793105 wasap.
CHOTA MAARIFA.
www.lacksontungaraza.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment