✍Watu wengi sana katika maisha tunapenda kufanikiwa... Kuishi maisha ya
kifahari, jamii kufahamu ya kwamba tupo, kupewa pongezi na watu mbali mbali.
Mbona sasa hatufikii hiyo hatua!! Nini tatizo jamani?
🏃 Unashindana na nani katika maisha
yako? Je! Ni rafiki yako au ndugu yako au jirani au mfanyakazi mwenzako? Ikiwa
upo katika mojawapo ya hayo makundi ya watu ambao wanashindana na wengne, basi
ndiyo maana hadi sasa bado maisha yako hayabadiliki. Unajitahidi sana kufanya
kila jambo na bado hufanikiwi... Ni kwasababu unashindana na wengne... Compete
with your own self.
🏃🏃Acha kushindana
na watu wengne katika maisha ya kupata mafanikio. Kila mtu ananjia yake ya
kufikia mafanikio... Njia aliyopitia Jack Ma tajiri wa China anayemiliki
Alibaba ni tofauti na njia aliyopitia Bill Gates mmiliki wa kampuni ya
Microsoft na njia tofauti na aliyoipitia Barack Obama.. Njia aliyoipitia
Reginald Mengi ni tofauti na ya Erick Shigongo au Barhesa na watu wengne wengi.
Hivyo ni vyema ukatambua njia yako ambayo ni Kushindana Na Unayemeona kwenye
Kioo Unapojiangalia.
✍🔎Anza
Leo kujichunguza vyema sana, kila mtu anaNafasi yake katika dunia hii. Nafasi
ya Nabii Eliya ilikuwa ni kudhihirisha ya kwamba yupo Mungu mwingne mwenye
uweza mkuu kuliko wa baali, Nyerere na Mandera Madiba walileta Uhuru na
Ukombozi wa Afrika... Nafasi yako ni ipi?
KILA MMOJA WETU ANANAFASI SAWA YA KULETA MAENDELEO KWA KUSIMAMIA KUSUDI LA YEYE KUWEPO HAPA DUNIANI. JIULIZE NI KWA JINSI GANI KAMA KIJANA UTAIHUDUMIA JAMII YAKO. |
📚Kila mtu anamaono na ndoto zake...hvyo hata
mbinu na Mipango atakayotumia kufika kule anapokwenda ni tofauti na wewe...
Unakuta kaweka Mipango ya kufungua salon, hoteli, kununua gari halafu nawe
unaiga na kufanya hvyo ili kumuonesha ya kwamba nawe unaweza... Hapo unapoteza
muda wako bure... Fanya kwako kwa ustadi mkubwa na utafanikiwa.
Mwambie huyo unayemwona kwenye Kioo ya kwamba
utamshinda katika masomo, biashara n.k..
COMPETE WITH YOURSELF NOT OTHERS.
Nakutakia Mafanikio mema.
©Lackson Tungaraza
0764793105 whatsApp group.
0 comments:
Post a Comment