Monday, December 14, 2015


Wahenga walisema,"UMOJA NI NGUVU" baada ya utafiti walioufanya katika nyanja mbalmbal ikiwemo kwa wadudu kama mchwa ambao licha ya udogo wao kimaumbile wanafanya maajabu kama ya kutengeneza vichuguu vikubwa na hata kula mbao na vitu mbalmbal vya thamani ambavyo ni vya aina hiyo.Hiyo yote kwa sababu ya "umoja" waliojijengea katika kazi.
Mara kwa mara tumekuwa tukikutana na wadudu njiani wakiwa kwenye misafara yao huku wamebeba nyasi, vijiti, maua n.k. kwa ajili ya ujenzi, chakula na matumizi mengine, kwa pamoja.

Katika nyanja ya biashara, pia mifano hiyo inahitajika ili kuweza kufanikisha kwa urahisi. chukulia mfano wa kawaida,ukiwa unahitaji kufyatua tofali 200 na ukawaalika rafiki zako 20 kukusaidia, kwa hakika hiyo shughuli utaimaliza kwa muda mfupi huku kila mtu akitumia nguvu kidogo. Lakini ikiwa mtu huyo huyo ataamua kufyatua tofali 200 mwenyewe, atatumia nguvu nyingi na muda mrefu kukamilisha hilo zoezi.

Biashara yoyote ile bila kujali ukubwa wake, ili ifanikiwe na kudumu kwa muda mrefu ni muhimu sana kuwa na UMOJA aidha wa mtu na mtu au taasisi na taasisi n.k. Hii ni kwa sababu kila mtu ana'nguvu' na 'udhaifu' wake, hivyo tunapokuja pamoja ule udhaifu unakuwa hauna nguvu wala kupata nafasi.Miongoni mwetu kuna watu ambao ni wazuri katika kupata mawazo mapya ya biashara lakini ni wadhaifu katika utekelezaji na wengine ni wazuri katika katika utendaji lakini hawana uwezo wa kupata mawazo mapya ya uendeshaji wa biashara n.k. Hivyo wakifanya shughuli pamoja wanaweza fika mbali sana ikiwa tu watafanya mambo yafuatayo;
1. Kutokuwa na majivuno
2. Kuwa na nidhamu na upendo

Chukulia mfano wa wafanya biashara wakubwa hapa nchini kama Bakhresa, Reginald Mengi na wengine wengi wameweza kupiga hatua kubwa kibiashara na kuliteka soko kwa muda mrefu kwa sababu ya UMOJA waliyoutengeneza na wafanya biashara wenzao na pia kufanya kazi na watu mbalmbal katika biashara zao wenye ujuzi mbalmbal kibiashara.

Watu wengi biashara zao hazikui au zinawahi kufa kwa sababu ya "Ubinafsi", wakidhani kila jambo wanaweza kulifanya na hata kama wakiliweza jambo hilo, unakuta muda mwingi umepotea hewani. Hivyo chukua notebook yako ukae sehemu tulivu utafakari haya;
1. Je, nina ushirikiano na wafanya biashara wenzangu wenye mitazamo chanya?
2. Je, nina penda kujifunza kwa waliotangulia kibiashara na kurekebisha makosa yao?
3. Je, biashara yangu inautofauti na biashara zingine ili kuleta mvuto kwa wateja?
Ukishapata majibu sahihi, chukua hatua. NGOJA NGOJA HUUMIZA MATUMBO.

Moja ya biashara ambazo kwa umoja na ushirikiano umewezesha wengi kufika mbali kiuchumi na kimtazamo ni biashara ya kisasa (Network Marketing). Lackson Tungaraza ni mmoja wa watu hao ambao wamepiga hatua kwa sababu ya kufanya biashara na watu wengine kwa umoja wakiwa na mitazamo chanya kwa pamoja.Unaweza wasiliana nae kwa sms/whatsapp kwa nambari 0764793105.

Hivyo kuanzia leo anza kutafuta rafiki wa kufanya nae biashara, lakini hakikisha pia nae ana mtazamo chanya na imani ya kuyafikia malengo yetu kwani wahuni ni wengi.

"USISAHAU, UMOJA NI NGUVU"
Au wewe unasemaje juu ya hili?..changia hapa na wengne wajifunze pia


UMOJA UNAFIKISHA WATU MBALI














Related Posts:

  • JIFUNZE JINSI YA KUTUMIA KINYWA CHAKO VIZURI NGUVU YA MANENO YATOKAYO KATIKA VINYWA VYETU Walisema manabii na mitume, “Atakaye kupenda maisha na kuona siku njema auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isinene hila” (1 Petro 3:10). Wengine wakaongezea”Mtu a… Read More
  • MAMBO MATATU MUHIMU ILI MTU AWEZE KUFANIKIWA. By Lackson Tungaraza 0764793105 whatsapp Hapo ulipo sahivi unaangaika kwasababu unataka Mafanikio, jiulize kwanza Mafanikio yana maana gani kwa upande wako!! Kila mmoja wetu anahitaji mafanikio katika mambo anayoyafany… Read More
  • SIRI INAYOVUTA MAFANIKIO SIRI INAYOVUTA MAFANIKIO  Nitakuwa muongo sana kama nikisema ya kwamba hamna mtu anayependa Mafanikio, hata wewe umechukua muda wako kusoma makala hii kwa sababu unapenda kufanikiwa kupitia hii Siri Inayovuta Mafa… Read More
  • KUWA STARRING WA MAISHA YAKO. ~Nilipokuwa mtoto nilipendelea sana kutazama muvi za ngumi ( action movies), katika kuangalia kwangu nilishangaa kuona ya kwamba muhusika mkuu wa Muvi ambaye ndiye anaitwa STARRING alikuwa hafi hata kama amekutana na maj… Read More
  • MAANA YA BIASHARA. Biashara ni mfumo wa ubadilishanaji wa huduma,yaani yule mwenye kitufulani anabadilishana na mwingine ili kuweza kuipata huduma hiyo. yaweza kuwa mali na hela au mali kwa mali. Kwasababu hiyo tunaona kuwa hapo awali kulikuwa… Read More

1 comment:

  1. Biashara za watu wengi zinachangamoto kubwa kutokana na ubinafsi na kukata tamaa mapema. Je wewe kwa mtazamo wako unawashauri nini wafanya biashara wengine?

    ReplyDelete

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI