Tuesday, September 1, 2015

Rafiki yangu msomaji naamini wewe ni mzima wa afya kwa namna moja au nyingne pia kila mmoja ana marafiki hata kama ni masikini au mfungwa.Lakini kiu yangu ni kukujuza ni kwa jinsi gani marafiki wamekufanya uwepo mahali hapo ulipo, inaweza ikawa ni kiuchumi au kivyovyote vile.Katika maisha kuna makundi mawili ya marafiki, naomba uchunguze kisha ujue rafiki ulionao wako kundi gani.


1:Wanaokwambia,
.."Huwezi kufanya hilo"
.."hiyo ni hatari,unajua ni wangapi wamefeli hiyo biashara?"
.."oh,nilishajaribu huko nyuma nikashindwa je wewe?"
.."kama ni wazo zuri unadhani hamna mwingine aliyekwisha fanya?"

2:Wanaokufariji,
.."Ndugu unaweza fanya,ni fursa nzuri kwako chukua hatua usichelewe".Biashara ya mtandao ndugu inakukutanisha na watu wa hili kundi la pili.
Tangu niwe mmoja wa hii familia ya BIASHARA YA MTANDAO maisha yangu yamebadilika kwani nimezungukwa na watu makini wenye malengo makubwa na imani ya kutimiza ndoto zao lkn pia elimu ya bure kabisa ya kifedha bila kulipia tofauti na biashara za kawaida utaingia gharama nyingi na kubwa za kuhudhuria mikutano ya kiujasiriamali na bado usipate mtu wa kukuongoza kufikia ndoto zako.Katika biashara hii ya mtandao unapewa mwongozo stahiki wa kukuongoza kuchukua hatua,kufanya na pia kuendelea kufanya kwa elimu sahihi.Ndugu "Biashara ya Mtandao" ni zaidi ya ofisi kwani unaifanya popote pale na unatembea na ofisi yako mkononi; mfano simu,ipad,komputa uliyonayo ni moja ya nyenzo ya kufanya biashara ya mtandao na utaweza kuwafikia maelfu ya wateja wako popote pale nchini kwa gharama nafuu ya MB za mtandao tu!!

#Ndani ya kila mtu kuna utajiri na umasikini,mchapakazi na mtegeaji.Sababu ya wewe kufanya biashara ya mtandao ni kwamba inasaidia au support utajiri uwezekushinda umasikini ulioko ndani yako kisha kusimama milele
..Ukitaka kufanikiwa kuwa karibu na marafiki waliofanikiwa usipende kujifunza kwa walioshindwa wanakuchelewesha kufikia lengo ambalo Mwenyezi Mungu ameweka ndani yako, tangu sasa chukua hatua ya maamuzi magumu ili ufanikiwe, tuko pamoja?

NDOTO!!
>>Kila mtu ana ndoto lakini sio kila mtu anaota.Naomba nikujuze juu ya aina tano za watu wenye ndoto maana kila mtu anasema ana ndoto lakini cha kushangaza bado ukiangalia wako palepale na wala maisha yao hayabadiliki.Tuwe pamoja sasa

1:Wenye ndoto za kale
..Hawa ni wale ambao unawakuta wanaongelea yaliyopita ktk maisha yao na jinsi walivyokuwa mashuhuri wakati huo.Mfano utasikia mtu akisema,"Wakati niko shuleni nilikuwa fundi wa Hesabu yaani hamna cha kunishinda" na ukimuuliza kwa sasa yuko wapi hajui

2:Wenye ndoto hafifu
..Hawa ni wale ambao unakuta wanamipango ya kufanya kila siku lakini hawafanyi na wanajitetea vilivyo, mfano atakwambia nikipata milioni moja nitafungua biashara.Sasa mwambie eti nakupa hiyo pesa sasa hivi ili uanze kufanya hio biasahara,atakwambia sahivi sina muda wa kutosha labda hadi mwakani.

3:Wanaotimiza ndoto zao lakini bado hawafurahi
..Hawa ni wale ambao kwa mfano kipindi wako shuleni utakuta wanakwambia nataka nikimaliza niwe Dokta lakini akishapata hiyo ajira anaishi maisha asiyoyapenda.Ikifika Jumapili usiku anakuwa na mawazo mengi kwasababu anajua Jumatatu asubuhi na mapema anahitajika ofisini na hawezi kuacha kwenda

4:Wenye ndoto kubwa maishani lakini kwa kukosa nyenzo za kupitia ili kutimiza ndoto zao bado wapo hapo hapo hadi leo.Hivyo ili mtu huyu afanikiwe inabidi awe karibu na timu ya watu wenye uelewa wa hilo jambo

5:Wenye ndoto kubwa na baada ya hizo ndoto kutimia wanaendelea tena na tena.hii ndio tofauti ya waliofanikiwa na wasiofanikiwa.
..ukitaka kufanikiwa jaribu kubadili ukubwa wa ndoto yako.Waliofanikiwa wanandoto kubwa tofauti na wengine.
..Inawezekana ukawa wewe ni muhanga wa kutokujua jinsi ya kutimiza ndoto zako, mimi pia nilikuwa hivyo mwanzo lakini BIASHARA YA MTANDAO/NETWORK MARKETING imenibadili kimtazamo lakini pia kifikra.Hujachelewa bado kwasababu unakokwenda ni pazuri zaidi ya ulikotoka ila tu hujajua.

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI