Binadamu kila siku tunatafuta mbinu za kuboresha maisha yetu kwa namna moja ama nyingine. Tatizo linakuja pale ambapo hatutambui ni mbinu gani ambazo ni sahihi kutofikisha kule tunakotaka kwenda au zipo sio sahihi ambazo zitaturudisha nyuma zaidi. Baada ya kulichunguza lini, leo tunaangalia kwa pamoja, mbinu kumi ambazo ukitumia utabadili na kuboresha maisha yako hatua kwa hatua. Hatua hizo ni;
1;JUA MAANA YA MAFANIKIO
..Wewe mwenyewe ndio unajua ni kitu gani unataka kwenye maisha.Andika malengo yako na bandika hata mlangoni uwe unayaona
2;PATA TASWIRA YA MAFANIKIO YAKO
>Mara kwa mara fikiria kama tayari umeshafikia maisha uliopanga kufikia.Kama ni biashara kubwa unatakiwa fikiria kama tayari unasimamia biashara hiyo
3;JIAMINI UNAWEZA KUFIKIA MALENGO NA MIPANGO YAKO
>Kuwa na imani kwenye uwezo mkubwa ulioko ndan yako.Amini licha ya vikwazo utakavyokutana navyo unaweza kufikia mafanikio makubwa,usijiwekee shaka hata kidogo
4;FIKIRIA MAKUBWA
>Mawazo yako ndio yatakupatia kile unachotaka,fikiria madogo na utapata madogo,fikiria makubwa na utapata makubwa.Mara zote kuwa na mawazo makubwa na chanya
5;KUWA NA MSIMAMO
>Ukishapanga mipango yakohakikisha unaifuata bila ya kuiacha/kuahirisha.Ukianza kuahirisha mambo utashindwa kufikia mafanikio, kama umeweka mpango wa kufanya jambo fulani lifanye kwa muda uliopanga.
6;WEKA VIPAUMBELE
>Huwezi kufanya kila kitu na wala huna muda huo.Hvyo weka vipaumbele vya mambo ambayo ukiyafanya yatakuletea mafanikio makubwa, yafanye hayo kwa ufanisi mkubwa
7;GAWA MAJUKUMU KWA WENGINE
>Kwa mambo yale ambayo huwez kuyafanya tafuta watu ambao wanaweza kuyafanya vizuri na wapatie kazi hizo.Hakikisha unaowapa majukumu hayo wanayafanya kwa ufanisi mkubwa
8;TAFUTA USHIRIKIANO
>Tafuta watu wenye malengo kama ya kwakona muende pamoja.Kama utakosa mwambie mtu unayemwamini awe anakufatilia,mwambie ni malengo gani umepanga na yeye awe anafuatilia kama kweli unafanya vile ulivyopanga
9;KUWA NA MOTISHA AU HAMASIKA
>Mara zote kuwa na njia za kujiamasisha.Safari inaweza kuwa ngumu sana ila kama una njia za kujiamashisha utaweza kuvuka vikwazo.Soma na sikiliza vitabu vya kuhamasisha
10;JIPONGEZE PALE UNAPOFIKIA MALENGO YAKO
>Binadamu tunapenda kupata pongezi.Hvyo kama ukiwa na njia ya kujipongeza itakupa hamasa ya kufanya zaid