Kwanza nawashukuru sana ndugu,jamaa na marafiki kwa kusoma makala mbalmbal ambazo ninakuwa nikipost facebook hakika ninyi ni watu wa muhimu sana na nina furahi sana.
..Nami leo nawarudishia fadhira zangu japo ni endelevu sio leo tu.Mimi binafsi "Lackson Tungaraza" nmepitia changamoto nyingi kufika hapa leo na nmegundua kuna mambo mbalmbal yanayopelea kutokufanikiwa na umeshayatenda lkn ngoja leo nikupe namna ya kushinda hivyo vikwazo na usonge mbele za spidi ya umeme..tuanze sasa pamoja:
1:ZUNGUMZA NA NAFSI YAKO KWA MANENO YA NGUVU
..Hapa ninakushauri ufanye mambo kwa kusikiliza msukumo wako na zaidi pale unapoona kushindwa ebu zungumza na nafsi.Mfano mimi huwa nachukua kioo halafu najiangalia ktk kioo na kusema " Lackson najua wewe ni shujaa, hii hali unayopitia ni ya muda tu na nina uhakika kati ya watu wenye mvuto na umuhimu ktk jamii ni wewe. Jamii inakutegemea wewe ukiacha nani atafanya?.." halafu ghafla napata tena msukumo ndani yangu. Hata wewe anza leo kwa kujiongelea mwenyewe ktk kioo chako baada muda fulani utanipa matokeo yake.
2:JARIBU KUZUNGUMZA NA WATU WALIOFANIKIWA KTK JAMBO UNALOHITAJI
..Hapa waulize ni kwa jinsi gani wameweza kufika hapo, nyakati nguvu walizokutana nazo, walipokosea wakati waanza safari ili upate mwanga.Usipende kuona tu dhahabu imeng'aa bila kujua imepitia wapi.Waswahili wanasema USIONE VYAELEA VIMEUNDWA.
3:FANYA WEWE MWENYEWE KWA KUJIAMINI
..Usiishi maisha ya kuiga mtu aliyefanikiwa, utakata tamaa pindi usipofanikiwa kama yeye kwa kupata matokeo sawa, hvyo baada ya kujifunza kutoka kwake hebu jaribu kuona jinsi ya kutumia hyo elimu wewe kwa matendo
4:LAZIMA UKUBALIANA NA MIMI, MAFANIKIO YANAHITAJI NGUVU NA KUTOKUKATA TAMAA
..Lazima ukubali ukweli kwamba ktk safari ya kujifunza utajisikia mwoga au kukatishwa tamaa.Jaribu kupiga hatua kila siku hata kama ni ndogo utafika
5:KILA MARA CHUNGUZA MALENGO YAKO KWA UFASAHA
..Unaweza andika malengo na mipango yako ya wiki,mwezi,mwaka n.k na ukabandika sehemu unayokaa muda mwingi au kupita mfano kwenye DRESSING TABLE,CHUMBAN MLANGONI n.k, hii itakusukuma kupambana zaidi kila utakapoona
6:SEMA HAPANA
..Kuna mambo au tabia unayojikuta unafanya pasipokujua au kutokufanya uwamuzi sahihi.Inawezekana umepanga ni muda kusoma kitabu fulani lkn anakuja rafiki yako na habari ya kwenda mpirani na wewe unaacha na kuondoka, hyo ni kutokujua kusema NO..kwanzia sasa jaribu kutaja neno NO ukiwa peke yako mara kwa mara na utakuwa imara tena
7:KABLA YA KUTATUA TATIZO JARIBU KUCHUNGUZA NJIA ZA KUTATUA
..Jaribu kuchunguza njia zaidi ya moja, Je ni sahihi kwa tatizo lako? usikurupuke kufanya maamuzi yako ya leo maana ndio matokeo ya kesho. Wazungu wanasema THINK TWICE BEFORE YOU ACT yaani fikiri kabla ya kutenda
MWISHO KABISA..Jipongeze kwa kila hatua unayopiga kufikia ndoto zako hata kama ni ndogo lkn si umesogea, ukijichukulia mtu wa maana bila kujidharau utafika mbali
Mawasiliano: 0764793105 kama una swali au unahitaji ushauri lkn pia unaweza kuni ADD kuwa rafiki yako "Lackson Tungaraza" au Whatsapp kwa hyohyo namba..
Ahsante sana kwa kusoma na ubarikiwe, tukutane tena muda mwingine kwa mada nzuri zaidi