FANYA KWA UTOFAUTI
Katika hii dunia hakuna jipya chini ya jua, ukiangalia mambo yote unayoyaona yanatokea tayali yameshafanywa na watu wengine huko nyuma, ukiangalia biashara zote unazoziona leo zimeshafanywa na watu wengine huko nyuma
. Swali linakuja moja tu hivi ni kweli uache kufanya
kwasababu wengine walishafanya? Tena huenda waliofanya walishidwa Siyo sahihi wewe kuacha kwasababu wengine walishafanya tena wakashindwa. Unachotakiwa kufanya wewe ni kufanya kwa tofauti , fanya tofauti na wao walivyofanya. Angalia wapi wao walikosea, halafu wewe rekebisha ufanye kwa utofauti.
Haijalishi mko wengi kiasi gani mnaofanya biashara sawa, wewe fanya kwa utofauti, hebu angalia leo hii, biashara zipo nyingi sana, watu wengi wanaogopa kuanzisha biashara kwasababu wanaona kila biashara wanazotaka kuanzisha tayali watu wameshaanzisha.
Haijalishi mko wengi kiasi gani mnaofanya biashara sawa, wewe fanya kwa utofauti, hebu angalia leo hii, biashara zipo nyingi sana, watu wengi wanaogopa kuanzisha biashara kwasababu wanaona kila biashara wanazotaka kuanzisha tayali watu wameshaanzisha.
Wanaogopa kufanya, huwa najifunza sana kutoka kwa msanii Diamond platnums, ni kweli wasaniii wapo wengi sana tena wengine wenye uwezo kuliko hata yeye lakini kitu kimoja tu yeye anachowashinda ni kufanya kazi zake kwa utofauti, hapo ndipo anaposhika soko la muziki.
Huwezi kuona amefanya kama alivyofanya wakati uliopita, huwezi kuona amefanya kama wengine
wanavyofanya. Tatizo kubwa
linalowakumba watu wengi ni kuwa wanafanya mambo
yaleyale, kwa njia zile zile,wakati ule ule na watu wale wale halafu wanataka kupata matokeo tofauti
haiwezekani.Lazima ukubali kufanya kwa utofauti utaona maajabu kwenye kitu ambacho wengine wamekikatia tamaa wewe ndio unafanikiwa.Biashara ambayo tunaifanya sisi na wajasiriamali wengine ambao tumeamua kuungana na kufanya pamoja ambapo hata wewe unanafasi ya kuungana nasisi kama unaroho kweli ya kijasiriamali na kutafuta mafanikio nitakupa nafasi hiyo.
Ni biashara ambayo
wengi wanaona kama ni ngumu, na ninakumbuka wakati sijaanza kuifanya hii biashara niliona kama ngumu,lakini nilipoamua kuingia kwenye biashara rasmi nilijisemea kitu kimoja tu, kuwa haijalishi watu wangapi wanafanya hii biashara mimi nataka kuifanya kwa utofauti.
Nilichogundua ndani ya biashara watu hawataki kuumiza vichwa kufanya kwa utofauti wanataka
kufanya kama wale wale walioshindwa ndio maana na wao wanashindwa. Ukiangalia watu wengi
sana wanaangalia na kujifunza kwa walioshindwa, unamwambia kuhusu biashara anakwambia hii alifanya mtu fulani akashindwa, hiyo ngumu sana.Sasa unajiuliza wewe ndio mtu fulani?
Wewe unaweza kufanya kwa utofauti na ukafanikiwa, ndio maana biashara nyingi watu wanaiga,kamuona jirani kafungua duka, na yeye anakurupuka anafungua vile vile.
TATIZO SIO KUFANYA
MAANA UNAWEZA KUFANYA NA UKAFANYA KAMA WALE WALE.TATIZO NI KUFANYA KWA UTOFAUTI.