Thursday, September 10, 2015

Kuna msemo watu wengi hupenda kusema ati kijana ni taifa la kesho .Mimi binafsi naona ni propaganda tu. Ewe kijana mafanikio yako ni sasa sio kesho kwani inaweza fika kesho na bado hali ni tete .kijana unapaswa kujifunza mambo ambayo yatakutoa kwenye umasikini..

MJASILIMALI ni mtu Yule ambaye anakuwa na uwezo wa kuyasoma mazingira na kuweza kuyatumia na kuyafanyia biashara, na ni mwepesi kuchangamkia fursa kuliko wengine,Pia ni mtu ambaye anauwezo wa kuthubutu, kubuni, kuanzisha na kuendesha biashara au mradi wa namna yoyote utakao mwingizia kipato chake.Tunasaidiana pamoja na wewe kufahamu mbinu mbalimbali ambazo zitakusaidia kujiajiri tuzisome pamoja

1. kijana unatakiwa kufahamu kuwa maisha yako unayetakiwa kuyaongoza na kuyastawisha ni
wewe mwenyewe na wala sio mtu mwingine kama Wazazi, marafiki au mamlaka yoyote , hao wengine watakusaidia kuyafikia yale uliyoyapanga kama kijana.


2 .JIAMINI, 
kikubwa kama kijana unatakiwa kujiamini katika yote uyapangayo na katika lolote ulitakalo kulifanya ili mradi tuu litaleta mabadiriko chanya katika maisha yako.

3. UWE MTAMBUZI WA FURSA, 
kijana unapaswa kuwa mtambuzi wa fursa ambazo zinakuzunguka na uwe na uwezo wa kuzitumia katika kujiajiri kwani dunia imejaa fursa nyingi
ambazo kama kijana unaweza kuzitumia na zikakuingizia kipato chako cha kila siku

4. JIFUNZE KUWEKEZA, 
unaweza ukawa unawekeza katika kipato lakini kikubwa jifunze kuwekeza katika fani mbalimbali ambazo zitakuwezesha katika kujiajiri , hivyo ujuzi na ufundi mbalimbali utakuwezesha wewe kuyafikia mafanikio yako katika maisha

5. WEKA DIRA NA MALENGO, 
hivi vitu vitakusukuma sana katika kuyafikia mafanikio yako katika kujiajiri kwani vitakuongoza pale unapotaka kuelekea na kuwa mbunifu zaidi katika yale
unayotakiwa kuyafikia

6. USIKATE TAMAA,
 unahitaji kuwa na moyo wa kijasiri zaidi kama kweli umedhamilia kuwa mjasiriamali kwani ni hatua ambayo unatakiwa kutokata tamaa kirahisi, maisha yamejaa changamoto nyingi sana katika dunia hauhitaji kukata tamaa.

7. ANZA MAHALI ULIPO,
 kijana hebu acha kujichelewesha na kusubirisha ndoto zako ,jifunze kuanza mahali ulipo, kwani katika maisha kuanza ndiyo  kitu muhimu

8. ONGEZA UVUMILIVU, 
mafanikio hayaji kwa siku moja kuwa mvumilivu, pindi unapotaka kuyafikia mafanikio.
NIKIWA NAPIGA KAZI OFISINI NEPSTAR

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI