Karibu sana
rafiki yangu mpendwa katika mfululizo wa masomo yangu kwa njia ya mtandao.
Wakati uliyopita, nilifundisha juu ya MTAJI KWA KIJANA NI UPI!! Maana neno
MTAJI limekuwa maarufu sana kwetu vijana hasa katika karne hii ya sayansi na
teknolojia/taarifa tofauti na karne ile ya viwanda [industrial age]. Kama
ulipitia somo hilo, nadhani utakuwa umepata jambo zuri sana la kuyafanya maisha
yako kuwa bora zaidi… Kama bado, soma hapa kwa kubofya maandishi haya: MTAJI KWA KIJANA NI UPI!!
Leo
tujifunze jambo jingine jipya ambao kwa nafasi yake litatusaidia kuwa makini
zaidi kuelekea katika maisha ya mafanikio, ambayo tunayaona katika fikra kila
tulalapo na tuamkapo. Karibu sasa, tuwe pamoja.
Ubunifu,
Kipaji, Karama au Uwezo uliyopo ndani yako huwa unaonekana zaidi unapokuwa karibu
na watu wengi[kwa kuongeza watu] au unapokuwa mwenyewe[unapokuwa faragha]?
Jiulize, Jijibu. Hii itakusaidia sana katika safari yako ya kuifikia Ndoto
iliyoko ndani yako ambayo Mungu kakupatia.
Kuna watu
ambao hadi sasa hawajaona Vipaji vyao vikiwaletea manufaa kwa sababu
hawajajichunguza, hawajajitathmini na kujitambua. Self-Discovery
is the foundation, it comes first and others follow.
Ukiona ya kwamba Ideas[mawazo] ya
kufanya mambo makubwa zinakuja ukiwa karibu na watu wengi kila mara, endelea
kufanya hivyo na uwe makini usipitwe. Ikiwa ni ukiwa mwenyewe chumbani kwako au
sehemu umepumzika, tia bidii katika Kujitenga na marafiki/watu ambao
wanakupotezea muda mwingi na utumie muda huo kuandika hizo ideas punde
zinapokuja ndani yako… Sir. Isack Newton aligundua ‘gravitational force’
alipokuwa amepumzika chini ya mti, WEWE JE?
Mara nyingi nimekuwa nikipata masomo
mbali mbali ya kufundisha hapa pamoja na kuwa mbunifu katika mambo mbali mbali
ninapokuwa faragha. Blog yangu hii {www.lacksontungaraza.blogspot.com} pamoja
na ile nyingine {jesusisalive2016.wordpress.com} nilizitengeneza wakati
nilipokuwa faragha, sikuweza kufanya hivyo nilipokuwa na watu wengi. Design
nyingi nimezifanya nikiwa peke yangu, tofauti na pale ninapokuwa karibu na watu
mbali mbali.
Nawe pia jitathmini vyema ili ujue ni
eneo gani unatakiwa kuliwekea nguvu na umakini mkubwa zaidi. Isiwe kwamba Mungu
anataka kukupa maarifa na ubunifu ukiwa peke yako, halafu wewe huo muda ndiyo
unautumia kutafuta watu wa kuchati nao mtandaoni au unaenda kwa jirani kutafuta
wa kupiga nae soga.
Kwa leo naomba kuishia hapa,
tutaendelea na somo hili wakati mwingine kama Mungu atakavyotujalia Uzima na
afya. Kama unambinu nyingine nzuri na unapenda jamii ifahamu, toa maoni yako
hapa {Comment}. Unaweza pia kunipata katika maeneo yafuatayo kwa ukaribu;
Facebook: www.facebook.com/ltungaraza
Youtube: www.youtube.com/c/LacksonTungaraza
Google Plus: www.google.com/+LacksonTungaraza
Twitter: @lacksonthecoach
Instagram: LACKSONTUNGARAZA
WhatsApp/sms: 0764793105
TWENTY YEARS TO COME BEGINS TODAY, MAKE EVERY MINUTE COUNTABLE.
WASTE NOT YOUR TIME
Lazima kieleweke.... toa maoni yako hapa
ReplyDelete