Tangu Uanze kuvunja Laana za
UMASKINI, huu ni Mwaka wa ngapi, na Je Umeshaanza kuwa TAJIRI?
Kabla ya Kuanza au
Kuendelea tena na Uvunjaji Wako wa Laana za UMASKINI, Tathimini Kwanza ni kwa
Jinsi Umejitoa Kulipa Gharama za kuwa TAJIRI; Muda, Nguvu, Fursa, Maarifa, Pesa
N.k
... Je Umeshahudhuria
Semina ngapi za Kiuchumi-za bure na za Kulipia,?
... Umeshasoma VITABU
vingapi vya Kukusaidia Katika eneo Unalotaka Kufanikiwa Kiuchumi,?
... Umeshajifunza kwa
Watu gani Waliyokutangulia,?
... Umeshaanza Kufanya
mangapi tangu Umalize Kusoma Vitabu na Kuhudhuria Semina Za Kiuchumi,?
... Matumizi Yako ya Kifedha Yakoje -Nidhamu ya Mapato na
Matumizi,?
... Matumizi Yako ya
Muda Yakoje - Tangu Unapoamka hadi Unaporudi Kulala,?
... Umetumiaje FURSA
ya Kifedha zinazokuzunguka,? Mfano Kutatua Matatizo na Changamoto zilizopo
kwenye Jamii Yako; Maji, Chakula, Usafiri, Elimu N.K.
... Umejitoa Kwa Kiasi
gani Kujifùnza kwenye Makosa Yako ya Awali,? - Kulalamika na Kuwalaumu Wengine
hakuleti Msaada wo Wote.
... Unatumiaje
Teknolojia ya Sasa katika Mambo Yako ya KIUCHUMI,?
-
"Ukiendelea Kuishi Wakati huu Sasa kama zamani, Utapata Shida sana
Kufanikiwa Kiuchumi. Kila Msimu Mpya Unapoingia, Jaribu Kubadilika kiMalengo na
Kimkakati, lakini ubaki kwenye MAONO Yako."
-
Lamax.
... Je, Una MAONO
Yaliyoandikwa,?
- Maono Ni dira ya
Maisha Yako... ni Wapi Uelekee na namna gani Uelekee huko.
- "Pasipo Maono
WATU HUACHA KUJIZUIA"
... Je, Una Mipango na
Mikakati gani ya Kujikomboa Kiuchumi,? - Hii inafuata baada ya Kuwa na Maono
Yaliyoandikwa.
Baada ya hapo, ndipo
Uendelee au Uache Mambo Yako ya KUVUNJA LAANA ZA UMASKINI. Inawezekana UJINGA
Wako ndio Unaowapatia UTAJIRI na UMAARUFU Wale Mitume na Manabii wa Uongo.
. Life Is a Choice
You Live What you Decide.
. LACKSON TUNGARAZA
0 comments:
Post a Comment