Monday, May 6, 2019


JAMBO KUBWA KABISA NA LA KWANZA NI KUJIANDAA NA KUWA TAYARI (Get prepared and Be Ready).

LEO UKIMWONA "Diamond Platinumz", au "Joel Nanauka" anapata nafasi ya Kuzunguka sehemu nyingi Unadhani ya kwamba ni Bahati tu!! Hapana kama ingekuwa ni Bahati tu hata wewe naye una bahati, lakini Mbona huchaguliwi‼.

NI LAZIMA UCHAGUE ENEO MOJAWAPO LA KIMAISHA AMBALO UNAJIWEKEZA HAPO KWA ASILIMIA MIA MOJA - KIASI KWAMBA HAKUNA FURSA UTAKAYOIKOSA KWENYE HIYO NAFASI.

- Shida yako kubwa ni kwamba Unataka kuwa "Superstar" wa Kila Kitu. Unataka Kila FURSA ya Kilimo, ya UIMBAJI, ya Uchekeshaji, ya kupiga kampeni za Siasa, ya kucheza Mpira, ya Kuigiza, ya kucheza Muziki, ya mitindo, n.k.

Sio Vibaya kuwa na UJUZI wa aina mbali mbali, Ila Unapaswa Kwanza kuwa vyema kwenye eneo Mojawapo. Christian Ronaldo (Cr7) sio kwamba hafanyi mambo mengine Mengi, Ila kajiwekeza zaidi kwenye Soka  (football) na ndio maana ameshachukua tuzo za Mchezaji bora wa Dunia Mara tano.

INA MAANA
Kama Umeamua kujikita kwenye Kilimo, Anza kwanza kwa Kujiwekeza kwa kina zaidi kwenye aina fulani ya Mazao kwa Sababu Mazao ni Mengi sana na yana Mambo Mengi sana ndani Yake. Kama ni kwenye Mahindi na Mihogo, basi Ujue kwa Undani zaidi kiasi kwamba Ikitokea kuwa Watu wanahitaji mtu wa kutoa Semina kwa wakulima wengine juu ya hayo Mazao, Unaichukua hiyo Fursa Fasta bila kujiuliza_uliza.



#MFANO WANGU MIMI LACKSON TUNGARAZA;

  Niliamua kujikita kwenye "UANDISHI na UALIMU" wa mambo yanayowahusu sana Vijana. Kiasi kwamba Wakati nilipokuwa UDOM Sikuwa mwepesi wa kuacha FURSA zinazokatiza kwenye hayo Maeneo. Kuna Wakati Nilikuwa Naenda kwenye Vikundi vya wanavyuo Wengine kama Watu Wengine Wanaoenda Kuhudhuria. Lakini Ghafla nasimamishwa kuongea na VIJANA hata kwa dakika 5. Na kwa lilikuwa ndiyo eneo nililolichagua, Nilikuwa Sikatai hizo nafasi, Nilikuwa nasimama na kushusha nondo kana kwamba nilikuwa nimeambiwa nijiandae.

Kuna Wakati Nilikuwa napewa taarifa wakati sherehe inaendelea. Kiongozi anakuja na kuniambia, "Lackson tunakupatia hapa dakika 5 za kusema na Vijana hapa kuhusiana na mambo ya Shule na maisha."Nami nikawa nafurahi sana kwa sababu ndizo FURSA ninazozitaka maishani - kupata vijana wa kusema nao maswala ya Kimaisha.

Unajua kuna Watu wanaosema ya kwamba wameitwa na Mungu kuwa Waimbaji. Lakini ghafla Ukiwaita kuimba, wanakuchukia kwa Sababu hukuwapa taarifa ili wajiandae.

     #Dr. Sunday Adelaja kwenye Kitabu chake cha WHO AM I? Alisema ya kwamba; Mojawapo ya njia Unayoweza kuitumia Kujua eneo uliloitiwa kumtumikia Mungu (kipaji, Kipawa,) ni kuangalia Uwezo Wako wa kufanya hilo jambo bila Kupewa muda wa kujiandaa. Ikiwa na maana ya kwamba, hata ukiamshwa saa tisa usiku kuimba, au Kuchora, Unapiga Kazi bila Kuomba poo.

KWA HIYO BILA KUJIANDAA LEO USIDHANI YA KWAMBA UTAKUJA KUPATA MUDA MZURI WA KUJIANDAA KWA SABABU KESHO HAITAWAHI KUFIKA.

Fanya Leo. Mambo ya Kulaza Viporo achana nayo. Mungu angekuwa analaza viporo, asingeweza kuimaliza kazi ya Uumbaji (Creation) ndani ya Siku 6. Kila Siku alikuwa anapiga kazi moja hadi kuimaliza kabisa katika Ubora aliyoutaka, na mwisho wa Siku ikaandiwa, "Mungu akaona Kila kitu alichokifanya, na tazama, ni Chema Sana."

Mwenye HEKIMA Mmoja aliwahi Kusema ya kwamba, "LIVE BY THE PRINCIPLE: THERE IS NEVER A BETTER TIME THAN NOW, AND A BETTER DAY THAN TODAY." Akimaanisha ya kwamba, "Ishi kwa hii kanuni: hakuna muda bora kuliko uliyonao Sasa, na hakuna Siku iliyo bora zaidi kuliko uliyonayo Leo."

Kesho haipo kwenye Kalenda. Kwenye Kalenda kuna Jumapili, Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi tu.

Naamini Kuna Jambo Zuri sana ulilojifunza mahali hapa, basi nakusihi sana ulifanyie kazi kwa Bidii ili Miaka 20 Ijayo usijejutia mambo ambayo hukuyafanyia kazi wakati ambao una Afya na Nguvu Tele. Na IKIWA UNAHITAJI VITABU VYA LACKSONTUNGARAZA basi Bofya hii LINK: https://wa.me/255764793105. Au tuma Ujumbe Wako Kwenye nambari +255 (0) 764 793 105 .
AMUA LEO KUWA WA TOFAUTI kwa kufanya kazi na Lackson Tungaraza.



0 comments:

Post a Comment

MAKUNDI YA MASOMO YETU

CHAGUA MASOMO HAPA

Powered by Blogger.

ZILIZOSOMWA ZAIDI