Kuna siku niliandika hapa juu ya mada
inayoitwa LIFE IS A PROCESS… Katika hiyo mada nilitoa mfano wa Mti ambao huanza
kama mche baada ya mbegu kuwekwa ardhini. Hakuna mti ambao umetokea tu kuwepo
hapo ulipo, ulianzia katika udogo sana… wengine wakaumwagilizia Maji kwa
kutegea lakini baadae ukafikia hatua hiyo licha ya kupigwa na upepo na mvua
nyingi.
Mada ya leo inawezekana ikawa ni mwendelezo wa
mada iliyopita kwa mtazamo wako au ikawa mpya kulingana na nitakavyoelezea. Inawezekana hapo ulipo umekata tamaa kwa hali
ya maisha unayopitia kama kukoswa ajira, kutengwa na ndugu zako, maombi
uliyomwomba Mungu hujajibiwa, magonjwa kila siku ni yako, pesa unazisikia tu
katika matangazo ya M-Pesa, kila wazo la biashara unalopata halifanikiwi…
MAISHA NI SAFARI NDEFU!
Lackson Tungaraza. Maisha Ni Safari ndefu. |
I have Never met a great
person with an easy past… Sijawahi kukutana na mtu aliyefanikiwa katika maisha ambaye
anahistoria ya kawaida isiyokuwa na changamoto. Hiyo yote ni Safari na katika
safari kunachombo cha Usafiri ambacho unatumia; Yaweza kuwa ni miguu, pikipiki,
baiskeli, gari, ndege au mabawa… kulingana na hivyo vyombo vya usafiri vilivyo,
ni vigumu kuwa na matokeo sawa. Mtu awezaye kuwa na nidhamu kubwa ya maisha ni
yule ambaye anafuata kila hatua ya kwenda mbele, na siyo kuruka hatua ili awahi
kufika. Nadhani umeshasikia habari za watu wanaojiunga na FREEMASON ili
watajirike, ni mfano wa watu ambao wanataka njia za mkato… KULALA MASKINI NA
KUAMKA TAJIRI! SITARAJII NAWE UWE MMOJA WAO
Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nafanya
NETWORK MARKETING, nilikutana na changamoto sana. Nilikuwa nauza pedi za
wanawake chuoni, stendi kuu ya Dodoma na kwa watu mbali mbali katika maeneo yao
ya kazi. Moja ya changamoto ilikuwa ni MALALAMIKO YA BEI ya kwamba iko juu
sana.. nikawa nawaza *Itawezekanaje bidhaa yenye ubora mkubwa
ilingane na bidhaa ya kawaida!!* Nikawapotezea na kutafuta watu
wengine. Baada ya changamoto kama hizo, ikaja akili mpya na kuandaa VIPEPERUSHI
na kupita navyo kwenye SUPERMARKET na PHARMACY. Hii njia ilinisaidia sana hadi
Pedi zikaisha, nikawa nimejuana na watu mbali mbali na kukuza kipato changu [ushuhuda mfupi wa Lackson Tungaraza]
Kwanini
nakuambia MAISHA NI SAFARI!! Nataka ujue ya kwamba hiyo hatua uliyofikia ni
katikati ya safari, je utarudi nyuma uanze upya tena au utaendelea ili ufike
malengo uliyojiwekea kwenye maisha? Inawezekana safari ya kufikia mafanikio
yako ni 100KM na sasa umefikisha 50KM. Ukirudi nyuma, ni sawa na umemaliza
100KM lakini haujafikia ulikotaka kwenda… ni sawa na kutoka Dodoma kwenda Dar
halafu unaghairi safari yako Morogoro na kurudi tena Dodoma kisa umeona ya
kwamba haufiki unakokwenda. SONGA MBELE, MAZURI ZAIDI YANAKUJA.
Mmiliki wa kampuni ya soda ya PEPSI
alifilisika mara tatu lakini alisonga mbele akiamini ipo siku atafika, na sasa
unakunywa soda yake. Bill Gates aliambiwa ya kwamba dunia inahitaji Kompyuta 5
tu, lakini yeye aliamini ya kwamba atatengeneza Kompyuta ambazo kila mtu
atakuwa na yake… Leo hii karibia kila mtu ana Kompyuta yake. MAISHA NI SAFARI
NDEFU, ENDELEA MBELE KWA SABABU UNAKARIBIA KUFIKA.
Whatsapp Group: 0764793105 [Lackson Tungaraza]
Facebook: www.facebook.com/ltungaraza
Instagram:
LACKSONTUNGARAZA
Twitter:
@lacksonthecoach
Ni yapi maoni yako kama kijana?
ReplyDeleteNi yapi maoni yako kama kijana?
ReplyDelete