--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ukiangalia kwa Umakini,
kuingia katika jambo lolote lile katika maisha yako kuna ugumu wake kuliko
kutoka;
i.
Ukitaka kuingia katika ukumbi wa
kuonesha mpira, itakubidi ukate tiketi ambayo utaipata baada ya kutoa kiasi fulani
cha pesa, lakini wakati wa kutoka hakuna anayekwambia ulipie
ii.
Ili upate nafasi ya kuingia Bungeni,
itakuhitaji uwe na mtu atakayekualika ambaye anajulikana humo bungeni au uwe ni
mfanyakazi wa bungeni au kiongozi wa serikali ambaye unahitajika bungeni. Pia
utafanyiwa ukaguzi wa hali ya juu sana wakati wa kuingia kuliko wakati wa
kutoka
iii.
Ili uweze kuingia katika maisha ya
Uanandoa; Itakubidi upate mwenzi sahihi, umchunguze vyema, ujitambulishe kwao
na katika nyumba ya ibada, utoe mahari, sherehe ya harusi kama hali inaruhusu
nk. Lakini wakati wa kutoka nje ya ndoa inaweza ikawa ni Talaka tu au bila
taarifa wala gharama yoyote ile
Ingia
katika Utendaji. Kama kuingia huwa kunaugumu wake kuliko kutoka, basi ujue ya kwamba
ni wachache sana wanaoingia katika Utendaji…. Ingia ili utende, siyo kuwa
mtazamaji.
Chukulia
mfano wa mbegu ya mahindi, isipoingia katika utendaji baada ya kuwekwa ardhini
hatuwezi kupita mmea wa Mhindi ambao utatupatia mahindi mengi.
--------------------------------------------------------------------------------
Je
unapenda Kuchora, Kuimba, Uandishi, Uigizaji, Kufundisha? Ingia katika
Utendaji. Kumbuka ya kwamba Punje isipofanya kazi iliyokusudiwa ardhini,
hatutopata mmea wa mhindi.
---------------------------------------------------------------------------------
Thamini
eneo ambalo Mungu amekuweka… shuleni, ofisini, mtaani. Usisubiri hadi uwe na
shahada au stashahada ya sanaa ndipo uanze kuigiza au kuchora… Ingia katika
Utendaji.
Mwanzo
huwa mgumu, anza kidogo kidogo… Haba nah aba hujaza kibaba. Kila aliyekiongozi
leo, jana alikuwa anaongozwa. Aliyemaarufu leo kuna wakati alikuwa hafaamiki…
Ingia katika utendaji.
Kuwa
na Baiskeli halafu hujui kuendesha, ni bora usiwenayo kwasababu utafanana na
yule ambaye hajui kabisa kuendesha. Haujifunzi kuendesha baiskeli kwa kucheza
mchezo wa mashindano ya baiskeli kwenye Kompyuta au kwa kusoma shuleni; Bali
kwa kuingia katika utendaji. Kama punje ya mhindi iinavyohitaji udongo, maji,
mwanga wa Jua, mbolea ili kukua vyema… Vivyo hivyo nawe pia utafanikiwa ikiwa
utakuwa karibu na watu sahihi ambao mnaendana, kusoma vitabu sahihi ili kupata
maarifa stahiki na pia kuwa na msukumo wa ndani wa kutenda (Burning desire).
Ingia
katika utendaji, anza na ulichonacho siyo vile ulivyopoteza au unavyotamani
kuja kupata. Value what you have Now, you’ll get what you don’t have Next.
ACTIONS
SPEAK LOUDER THAN WORDS
Natumaini ya kwamba
utakuwa umepata maarifa ya kukusaidia kufikia ile ndoto kubwa unayotamani kuitimiza katika maisha yako.. aidha
kuwa mwanasoka bora Afrika, kuwa Mwigizaji mkubwa duniani, kuwa Mwimbaji wa
nyimbo za Injili au kuwa T.O [Tanzania One].
================================================
Kwa sasa Nimekwisha
kuandika Kitabu kingine kiitwacho KIJANA TAMBUA NAFASI YAKO. Inawezekana
kabisa Mungu amekupangia kuwa Mwanasiasa ili uikomboe nchi yako katika masuala
ya siasa safi na hadi sahivi haupendi siasa na unang’ang’ania kuwa Rubani au
Mwalimu yaani unachengana na NAFASI YAKO… Nafasi Yako inasifa mbili kuu,
kujenga ufalme wa Mungu na kuleta maendeleo katika jamii yako siyo kwako tu.
Utaijuaje Nafasi Yako? Kitabu hiki kitakupa Njia mbali mbali za kufuata katika
kutambua Nafasi Yako… YOU WERE BORN TO WIN NOT TO LOSE. Unaweza ukashiriki
katika Uchapishaji wa Kitabu hiki ili kiwahi kutoka kwa kutoa kiasi chochote
cha fedha kama ambavyo Mungu atasema nawe. Utautuma katika Namba yangu ya Vodacom
0764793105 [Lackson Tungaraza] na kisha utanipatia na jina lako kamili
ili nikuweke katika kumbu kumbu ya watu waliyofanikisha zoezi hilo.
=============================**=================
Ubarikiwe sana na
Mungu, uwe na siku njema.
Kwa Maoni na Ushauri:
0764793105 [WhatsApp/sms].
www.facebook.com/ltungaraza
Nini maoni Yako juu ya hii mada ukilinganisha na ulivyokuwa ukichukulia mambo katika maisha yako?
ReplyDeletekaribu sana katika uchangiaji wa mada