By
Lackson Tungaraza
0764793105
whatsapp
Hapo ulipo sahivi
unaangaika kwasababu unataka Mafanikio, jiulize kwanza Mafanikio yana maana
gani kwa upande wako!! Kila mmoja wetu anahitaji mafanikio katika mambo
anayoyafanya; Mwanafunzi, mwalimu, mwajiri, mwajiriwa, viongozi mbali mbali wa
kiserikali na wa kidini, vijana, wazee , wote wanahitaji mafanikio kwa viwango
tofauti tofauti kulingana na msukumo uliomo ndani ya mtu juu kile
anachokihitaji. Mimi mwenyewe Lackson Tungaraza ninayeandika haya, ninahitaji
mafanikio na ndiyo maana ninapenda na wewe uwe pamoja nami katika kupata
mafanikio stahiki. Mafanikio hayaji bila kufahamu njia ya kupitia, leo nitakupa
Mambo Matatu Muhimu ili uweze Kufanikiwa;
§ Watu;
Watu ni rasilimali
kubwa sana katika jamii yoyote ile ili iweze kuendelea. Bila watu kusingekuwa
na haja ya kufanya mapinduzi ya kisiasa au kibiashara. Ili ujue umuhimu wa watu
katika kuleta mabadiliko yoyoye yale katika jamii, fikiria ambavyo vyama mbali
mbali vya kisiasa vinatumia gharama kubwa kutafuta wafuasi kabla na baada ya
Chaguzi mbali mbali. Watu mbali mbali pia wamepata nguvu za Ushawishi katika
jamii kwa sababu ya kuwa na watu ambao ni wafuasi wake, nawe pia unahitajika
kuwa na watu ili uweze kufanikiwa katika hiyo biashara, dhehebu, shule, kampuni
yako n.k. Hivyo tengeneza urafiki na watu mbali mbali katika jamii ili uweze
kuyafikia mafanikio yako
§ Watu sahihi
Baada ya kuwa umepata
watu mbali mbali katika jamii, ni wakati sasa wa kufuata hatua hii ya pili ya kuwa
na watu sahihi. 75% ya yale ambayo watu wanayo na wanayoyafanya, yanatokana
na ushawishi wa watu ambao wanaambatana nao. Kuwa watu walioingia vyuo vikuu
wakiwa na tabia njema lakini bada ya kuanza kuambatana na watu wasio sahihi,
tabia zao zikabadilika na kuwa hatarishi zaidi. Wengine pia walizaliwa katika
familia ya watu maskini lakini wakapata bahati ya kuwa karibu na watu wanaotoka
katika familia zenye maendeleo ya kiuchumi, nao wakaanza kubadilika mitazamo
yao na baadaye kufanikiwa. Vivyo hivyo inakubidi nawe uchague watu ambao ni
sahihi kati ya hao ulionao, siyo kila rafiki ni sahihi. Ambatana na watu ambao
watakuwezesha kuyafikia mafanikio, kuanzia hapo ulipo na hata katika mitandao
ya kijamii. Usipokuwa na watu sahihi, utachelewa kufikia mafanikio au usifanikiwe
kabisa.
§ Taarifa Sahihi
Taarifa pia unazopata
kutoka kwa watu hao, inabidi iwe sahihi. Watu wengi wamekimbia ndoa zao,
biashara zao, wokovu, shule kwa sababu ya kupokea taarifa zisizo sahihi kutoka
kwa watu waliokuwa karibu nao. Unapopata taarifa fulani, jaribu kuichunguza
kama ni sahihi kwasababu inaweza kukuinua au kukuangamiza kabisa. Siyo kila
taarifa ni ya kuiweka moyoni au katika utekelezaji, chambua zinazokufaa katika
eneo lako unalotaka kufanikiwa. Tafuta taarifa za kibiashara kama unafanya
biashara au unataka kuwa mfanyabiashara, taarifa za wokovu wa kweli kama
unataka kumtumikia Mungu, taarifa za udaktari kama unataka kuja kuwa daktari au
kama wewe ni daktari n.k. Kuwa makini sana katika mambo haya Matatu ili uweze
kuyafikia mafanikio stahiki.
Natumaini utakuwa
umejifunza jambo fulani ambalo litakupa hatua zaidi kuelekea katika ulimwengu
wa mafanikio, sambaza somo hili kwa rafiki zako mbali mbali ili nao pia wapate
kujifunza (share). Ubarikiwe sana na uwe na siku njema.
0 comments:
Post a Comment