Thursday, October 1, 2015
- 7:44:00 PM
- Lackson Tungaraza
- BIASHARA YA MTANDAO
- No comments
Leo ni imani yangu hili somo litakutoa hatua moja hadi nyingne aidha ulikuwa unafanya hii biashara au ndipo unahitaji kuanza.Tuanze pamoja..
Ndugu yangu nimetumaini yangu unapokuwa unasoma hii makala umekata tamaa kabisa,
unataka kuirisha safari , hupati matokeo katika biashara yako, unatumia pesa nyingi kujaribu kuwafikia wengine waliotangulia. Kuna usemi mmoja unasema"Wafanya biashara
wengi wa biashara ya mtandao hupenda kupata pesa kubwa lakini wengi hawapati milele na milele" Mbali na hivyo waasisi wa biashara hii wanasema"Wafanya biashara wengi wa biashara ya mtandao hutumia pesa nyingi kufanikisha biashara zao kuliko pesa anayoingiza ktk biashara yake" Haya yote utaendelea kuyapata kama usipoepuka haya hapa katika biashara yako:
1.KUACHA KUFUATILIA KILE UNACHOFINDISHWA NA KUKIWEKA KWENYE VITENDO.
Katika kundi hili la biashara, ni kundi pekee linalokuwa linakupa mbinu nyingi za kibiashara, masomo mengi ya kibiashara, hivyo kuna wengine masomo huwazidia na kubaki hawana kitu chochote walichojifunza. Hii ni ishara kuwa biashara hii unaifanya kulingana na unavyojua wewe sio unafundishwa kufanya nini, hapo miaka yote utaendelea kusumbuka na hutapata ufumbuzi kamwe maishani mwako. Siri kubwa niliyojifunza ni kuhakikisha vitu vyote vidogo vidogo ninavyojifunza navitekeleza kwa vitendo kabisa.Je wewe unafanya hivyo? Kama hufanyi ndio maana kipato kinashuka badala ya kupanda, basi km mbinu zako unazozijua zimeshindwa kufanya kazi jaribu
hizi ninazokufundisha nina uhakika utabadirika kabisa kama mimi LACKSON nilivyobadilika.
2.Kutoipa kipaumbele hii biashara, na kuzingatia kile unachokifanya.
Biashara hii wengi wetu huwa wanaifanya kama maigizo,
leo ipo kwenye segment ya kuvutia kesho kwenye segment mbaya isiyomvutia mtazamaji.Jiulize kwa nini unapoteza muda wako kwa kutokuwa makini na unachokifanya.Hakikisha biashara yako unaipa kipaumbele kwani wenye mafanikio wote huweka nguvu nyingi kwenye Kitu kimoja hadi watakapo fanikiwa , nimekuwa nikifanya biashara yangu kama vile nimewekeza pesa kubwa sana, ndio maana siku zote napata matunda makubwa ukilinganisha na pesa niliyowekeza.Je wewe unangoja nini rafiki kiupa kipaumbele biashara yako? Hakikisha unabadilika katika mambo hayo kubadili kipato chako kuanzia mwezi huu
3.Kuhitaji kila kitu ufanye kwa msukumo.
Katika maisha ya kile siku kuna misukumo ya aina mbili, kutokana na jinsi gani msukumo huo unapatikana.Kuna msukumo wa nje, huu ni msukumo unaopatikana kwa kusikiliza, ujumbe wa sauti au picha au kusikiliza hotuba ya kibiashara wengi wetu
aina hii ya msukumo hupatikana watu wa aina kuu zifuatazo.
~Watu wanaopata msukumo na kufanya hapo hapo biashara kwa vitendo, lakini hawa msukumo hupotea ndani ya muda mfupi na kuacha.
~Watu ambao hawachukui vitendo pale pale huamua kwenda nyumbani na kujifikiria huchukua maamuzi polepole na baada ya muda huchukua maamuzi.
~Watu wanaochukua maamuzi pale pale na kufanya biashara polepole lakini kamwe huwa hawakati tamaa
~Watu ambao hupata msukumo lakini hakuna hata siku moja wamechukua hatua kwani ni Waoga
kukabili mchakato wa Mafanikio huwa siku zote wanaona ni safari ndefu wanabaki na ndoto zao.Hawa ndio makundi manne ya watu katika biashara ya mtandao ambao nimegundua wapo. Je wewe upo kundi gani? Hawa ndio siku zote hawezi kufanya biashara bila msukumo kutoka kwa kiongozi wa juu .Mfano, watu wengi nimekuja kugundua kuwa HAWAJITEGEMEI KIMAWAZO NA KIUTENDAJI kwasababu mwalimu wako au upliner wako amebanwa na majukumu basi na wao wanadhoofika kibiashara hilo ni tatizo kubwa sana. Unachotakiwa kukifanya ni kuwa mtu unayejiendesha kibiashara BILA KUHITAJI MSUKUMO WA NJE, UTASHANGAA MATUNDA YAKE NDANI YA MIEZI MICHACHE TU.
Kuna watu wenye msukumo wa ndani ya kufanya jambo (internal belief) hawa watu huwa nawaita MAHODARI kwani haijalishi anapata misukosuko gani siku zote huwa anapiga gwaride kuelekea mafanikio bila kukata tamaa.Watu wengi huwa wananiuliza, hivi bado unafanyabiashara yako ile ya siku zote?Huwa nawajibu NDIYO maana sijafikia ndoto zangu nilizojiwekea. Hawa watu huwa wanajiendesha AUTOMATIC yani bila msukumo kibiashara, sasa nataka nikwambie njia pekee ya kuwa na msukumo huu kibiashara ni KUTOJILINGANISHA NA WENZAKO, HAIJALISHI ALISHINDWA KUFANIKIWA LAKINI WEWE UNA ASILIMIA 100 ZA KUFANIKIWA, HAIJALISHI ALISHINDWA KUFIKA MAHALI FULANI KIBIASHARA HUYO SIO WEWE JIAMINI WEWE UTAFIKA.
Haijalishi unaona wenzako wamefika mbali kibiashara Haijalishi weka Juhudi bila Kujali wewe upo sehemu gani kikubwa kama umejiwekea lazima kila mwezi ununue mzigo wa dola 100/200 na lazima unahakikisha umezifikisha kwa nguvu zote , akili zako zote.Najua hizo ni NYUFA ZA KILA MFANYA BIASHARA katika biashara hii ya mtandao, basi ningependa nikwambie kuwa, ukitaka maneno haya yabadilishe kipato chako kuanzia leo, hebu yaweke kwenye utekelezaji haya utafurahia akaunti yako itakavyokuwa imejaa pesa tofauti na ilivyokuwa kabla hujabadili mtazamo kwa kusoma makala hii.
Najua kuna wengine hawatazingatia yanayosemwa humu, lakini kumbuka pia wachache wale ambao wana ndoto kubwa na waliamua kufanya hii biashara ili kutoka hatua moja kwenda nyingine watajua ukweli na umuhimu wa utekelezaji wa mambo haya makuu matatu ambayo mimi hakika yamekuwa ndio nguzo yangu.Hebu mwezi huu uwe mwezi wa mafanikio, chochote ulichopanga anza utekelezaji, umeumbiwa mafanikio, mamlaka yote yapo mkononi mwako, BADILI MTAZAMO KATIKA MIHIMILI MIKUU MITATU INAYOSABABISHA UFA KATIKA BIASHARA YAKO.
SOMA: http://lacksontungaraza.blogspot.com/2015/09/ kwanini-biashara-ya-mtandao.html
BAADA YA KUSOMA MAKALA HII NAAMINI UNASHAUKU YA KUFANYA HII BIASHARA LAKIN UNAMASHAKA UANZIE WAPI. HATA MIMI NILIKUWA HIVYO ILA NILIULIZA, KWAHYO CHUKUA HATUA YA KUPATA MAELEKEZO NA MBINU KUJIUNGA KUANZA BIASHARA YAKO LEO KWA GHARAMA NDOGO YA Tsh.26000/- LAKIN UWEKEZAJI MKUBWA AMBAO PIA MAMILIONEA WALIANZIA.
0764793105(sms/call/Whatsapp)
0 comments:
Post a Comment